Waziri wa Nishati, Dk. Medard Kalemani akizungumza na watumishi wa TANESCO Mkoa wa Shinyanga, leo katika ukumbi wa Mkuu wa Mkoa huo.
Na Marco Maduhu, Shinyanga
Waziri wa Nishati, Dk. Medard Kalemani, amelionya Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), kuacha tabia ya kukata umeme hovyo, huku mameneja wa shirika hilo wakitakiwa kuwatambua wateja halali wanaotumia nishati ya umeme ifikapo Januari 31 mwakani, pamoja na kuwafichua wezi wa umeme na kuwachukulia hatua..
Dk. Kalemani ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Chato mkoani Geita ametoa onyo hilo leo Desemba 30, 2020 katika ziara yake mkoani Shinyanga wakati akizungumza na watumishi wa Shirika hilo mkoani humo.
Katika ziara hiyo, Dk. Kalemani aliambatana na Naibu Waziri Steven Byabato, Kaimu Kamishina wa Nishati, Edson Wingabo, Kaimu Meneja Mwandamizi Rasilimali Watu Tanesco makao makuu, Festo Mkolla pamoja na Kaimu Meneja Mwandamizi wa Tanesco Kanda ya Magharibi, Mhandisi John Kiduko.
Waziri Kalemani amesema kitendo cha kukata umeme hovyo tena bila taarifa hapendezwi nacho na kubainisha tabia hiyo itakuja kumfukuzisha mtu kazi.
"Naombeni sana mameneja wa TANESCO nchi nzima acheni tabia ya kukata umeme hovyo, tena wakati mwingine bila hata kutoa taarifa , fanyeni kazi zenu kwa ufanisi, na eneo ambalo halina umeme mna hatarisha usalama" amesema Kalemani.
Pia amewataka wafanyakazi hao waache kufanya kazi kimazoea, bali wabadilike na kufanya kazi kwa kasi, ubunifu, na kwa usahihi, ili kutoa huduma stahiki ya usambazaji umeme kwa wananchi.
"Fanyeni kazi zenu kwa ufanisi kama mlivyofanya kwenye miaka mitano iliyopita mmefanya kazi vizuri sana, na hii ilitusaidia sisi wagombea wa CCM kweye kipindi cha Kampeni katika uchaguzi mkuu uliopita, kunadi sera zetu kwa wananchi na hatimaye kupata ushindi wa kishindo kutokana na TANESCO kufanya kazi vizuri ya kusambaza Nishati ya umeme kwenye maeneo mengi," ameeleza Kalemani.
Katika hatua nyingine, amewaonya watumishi hao kuacha kutoa lugha uchafu kwa wateja, pamoja na kuacha kujihusisha kufanya kazi na vishoka, huku akitoa miezi mitatu ndani ya mkoa huo wananchi wote wawe wamesha sambaziwa huduma ya umeme.
Kwa upande wake Naibu Waziri wa Nishati, Steven Byabato, amekazia suala la kuwabainisha wateja halali wanaotumia nishati ya umeme watambuliwe ifikapo Januari 31 mwakani, pamoja na kuwafichua wezi wa umeme na kuwachukulia hatua.
Naye Kaimu Meneja Mwandamizi Rasilimali Watu TANESCO Makao Makuu, Festo Mkolla, amesema kuwa maagizo yote ambayo yametolewa na viongozi hao atayafanyia kazi ili kuongeza ufanisi wa utendaji kazi kwa watumishi wa shirika hilo.
TAZAMA PICHA HAPA CHINI
Waziri wa Nishati, Dk. Medard Kalemani akizungumza na watumishi wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa wa Shinyanga (hawapo pichani) wakati wa ziara yake leo mkoani hapo.
Naibu Waziri wa Nishati, Steven Byabato akizungumza kwenye kikao na watumishi wa TANESCO Mkoa wa Shinyanga.
Kaimu Meneja Rasilimali Watu Mwandamizi TANESCO Makao Makuu, Festo Mkolla akizungumza katika kikao hicho.
Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga, Beda Chamatata akizungumza katika kikao hicho.
Watumishi wa TANESCO Mkoa wa Shinyanga wakiwa kwenye kikao chao na Waziri wa Nishati, Dk. Medard Kalemani.
Watumishi wa TANESCO Mkoa wa Shinyanga wakiwa kwenye kikao chao na Waziri wa Nishati, Dk. Medard Kalemani.
Watumishi wa TANESCO Mkoa wa Shinyanga wakiwa kwenye kikao chao na Waziri wa Nishati Dkr Medard Kalemani.