Waziri wa Katiba na
Sheria, Dk. Mwigulu Nchemba akizungumza na Kamati ya Ulinzi na
Usalama (hawapo pichani) ya Wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga kuhusiana kuchunguza upya
tukio la kumwagiwa tindikali, Spensioza Sylvesta mwaka 2015.
Na Salvatory Ntandu, Kahama
Waziri wa Katiba na Sheria,Dk Mwigulu Lameck Nchemba ameiagiza Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga kuchunguza upya shambulio la kumwagiwa tindikali, Bi Spensioza Sylivesta sambamba na kusitishwa kwa uuzwaji wa mali zinazomilikiwa baina yake na mmewe Richard Majenga kutokana na wawili hao kuwa na kesi mahakamani.
Waziri wa Katiba na Sheria,Dk Mwigulu Lameck Nchemba ameiagiza Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga kuchunguza upya shambulio la kumwagiwa tindikali, Bi Spensioza Sylivesta sambamba na kusitishwa kwa uuzwaji wa mali zinazomilikiwa baina yake na mmewe Richard Majenga kutokana na wawili hao kuwa na kesi mahakamani.
Agizo hilo alilitoa Jana Wilayani humo baada ya kusikiliza malalamiko ya Spensioza akimtuhumu mume wake Richard Majenga, kujaribu kumua kwa kumwagia Tindikali mwaka 2015 baada ya kutengana kwa lengo la kumiliki mali mbalimbali walizokuwa wanazimiliki zikiwemo nyumba, magari, shule na wiwanja.
Dk. Nchemba aliitaka Kamati hiyo kuhakikisha inachunguza tukio hilo kwa kina na kumpatia taarifa ikiwa ni pamoja na kuzuia uuzwaji wa Magari unafanywa na Richard Majenga wakati bado kesi iliyofunguliwa dhidi yake ikiendelea kusikilizwa na Mahakama.
“Fanyeni Uchunguzi wakina wakamateni wote waliohusika na tukio hili haiwezekani katika serikali hii mtu afanya jaribio la Mauaji ambayo yamesababisha ulemavu Mama huyu,halafu hatua stahiki za kisheria hazikuchukuliwa,”alisema Nchemba.
Sambamba na hilo Dk Nchemba aliitaka kamti hiyo kufualilia na kuzikamata mali na watu wote walionunua Magari,nyumba na viwanja zilizouzwa kinyemela na Richard Majenga ili haki ya Mama huyo ambaye kwa sasa amekuwa mlemavu ili iweze kupatikana kama sheria za nchi zinavyoelekeza.
“Nimetoka Dodoma kwaajili ya kusikiliza kero za Mama huyo,nimebaini kuna uzembe ulifanyika,kamwe sheria zetu haziwezi kupindishwa na watu wenye fedha ambao wanataka kuwanyanyasa wanyonge,katika hili naawahidi nitalifuatilia kwa makini hakikisheni mnatimiza wajibu,”alisema Nchemba.
Awali akizungumza katika Kikao hicho Bi Spensioza Sylivesta Mkazi wa Mtaa wa Nyakato Kahama alisema kuwa alimwagiwa tindikali mwaka 2015 akiwa na katika matembezi na watu wasiojulikana baada ya kuengana na Mume wake kutokana na mgogoro wa umiliki wa Mali walizozitafu pindi walipokuwa wanaishi pamoja.
“Baada ya kupata madhara ya Tindikali familia yangu ilifanya uchunguzi na kubaini watu waliotekeleza tukio hilo walitumwa na mume wangu ili aniue na yeye amiliki mali tulizochuma pamoja,baada ya mimi kupona nilifuatilia suala hili kwenye vyombo vya sheria lakini sikupata msaada,”alisema Sylivesta.
Nae Mkuu wa Wilaya ya Kahama Anamringi Macha aliahidi kutekeleza Agizo ili kuhakikisha haki ya Bi Spensioza inapatikana na taarifa ya uchunguzi wa tukio hilo ikikamilika itawasilishwa Kwa Waziri Dk Nchemba.
Waziri Nchemba akisaini kitabu cha wageni baada ya kuwasili wilayani Kahama
Waziri wa Katiba na
Sheria,Dk Mwigulu Lameck Nchemba akizungumza na Kamati ya Ulinzi na
Usalama ya Wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga kuhusiana kuchunguza upya
tukio la kumwagiwa tindikali Bi,Spensioza Sylvesta mwaka 2015
Waziri Nchemba akizungumza na viongozi wa halmashauri ya wilaya ya Kahama baada ya kuwasili kwa ziara ya siku moja wilayani humo jana