Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Shinyanga Vijijini Bi Ernestina Richard akipada mti katika shule ya Msingi Bulambila kata ya Mwalukwa, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 44 ya (CCM).
Katika kuelekea Maadhimisho ya Miaka 44 ya kuzaliwa kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) nchini
hapo February 5 Jumuiya ya Wazazi wilaya ya Shinyanga Mjini imeadhimisha kwa
kufanya shughuli za kijamii ikiwemo kupanda miti katika eneo la Shule ya Msingi
Bulambila na Sekondari ya Mwalukwa katika kata ya Mwalukwa.
Akiongoza zoezi la Upandaji miti Katibu wa (CCM) Wilaya ya Shinyanga Vijijini Bi Ernestina
Richard amesema kuwa miaka 44 ya chama cha Mapinduzi nchini wanajivunia mafanikio makubwa katika Nyanja mbalimbali
ikiwemo uboreshaji wa sekta ya Afya,Elimu Miundombinu ya Barabara, Umeme
Vijijini na Maji.
Ernestina amesema Chama Cha Mapinduzi kimeweza kuleta
mageuzi Makubwa nchini ukilinganisha na miaka ya nyuma ambapo hali ilikuwa tofauti
na miaka ya hivi karibuni kwani kiwango cha hali ya uchumi ilikuwa kawaida sana
ambapo sasa taifa linakimbia.
Aidha ameongeza kuwa maadhimisho ya mwaka huu
yameadhimishwa kwa mfumo tofauti kwa kufanya kazi za kijamii kwani jumuiya ya
wazazi inayo jukumu la kukuza maadili na umuhimu wa utunzaji wa mazingira ndo
maana wameamua kuadhimisha kwa kupanda miti ambayo ni zaidi ya 1000
Bi Ernestina amebainisha kuwa chama chake kitaendelea kusimamia utekelezaji
wa ilani kwa kuhakikisha miundombinu ya
elimu,elimu, maji na mengine inaimarika ambapo maadhimisho hayo
yanayawakumbusha kufuatilia utekelezaji wa ilani ambayo imebainishwa kitabu cha
ilani ya 2020-2025 ili iweze kufikiwa vizuri
Akieleza ahadi za Mheshimiwa mbunge wa Jimbo hilo Ahmed
Salum ambaye amepata dharura amesema kuwa mbunge huyo ametoa ahadi ya mifuko 50
ya saruji kwa ajili ya ukamalishaji wa ujenzi wa matundu ya Vyoo 14 katika shule ya Msingi Bulambila ambayo
yameanza kujengwa kwa nguvu za wananchi pamoja na mifuko 50 kwa ajili ya ujenzi wa zahabnati ya kijiji cha Ng”ang”a
Katibu huyo amewaongza wananchi kwa ushiriki wao mzuri
kwenye miradi ya maendeleo kwa kujitoa katika michango mbalimbali ikiwemo
ujenzi wa madarasa,matundu ya vyoo na
zahanati.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya wazazi Wilaya ya Shinyanga
Vijijini Peter Kawiza amesema kuwa wao kama jumuiya ya wazazi wameamua
kuadhimisha kwa kufanya shughuli za kijamii ambapo ameeleza kuwa suala la
changamoto zilizopo kwenye jamii bado zinaendlea kufanyiwa kazi kwani serikali
imeendelea kufanya vizuri kwa kutatua kero za wananchi
Mheshimiwa Peter amesema kuwa licha ya uwepo wa baadhi ya
changamoto katika jamii lakini chama na serikali kwa pamoja wanaendelea
kupambana kutatua kero hizo
Ameongeza kuwa jumuiya uandaa watu katika hatua mbalimbali
ikiwemo malezi, elimu na kua viongozi wazuri wa baadaae amabao watakuja
kulitumikia taifa ili iwe na vijana wazuri waloandaliwa kwa uzuri
Kwa upande wake mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya
Shinyanga vijijini ambaye pia ni diwani wa kata ya Mwalukwa Bw. Ngasa Mboje
amesema kuwa serikali ya chama cha mapinduzi inaendelea na utatuzi wa
changamoto zinazowakabili wananchi wa
kata ya Mwalukwa ikiwemo uhaba wa Maji
na umeme kwa baadhi ya vijijini ambavyo havijapata umeme.
Ngassa amesema kuwa shughuli nyingi zinazofanywa katika
Kata yake zinafaywa kwa nguvu za wananchi ikiwemo michango mbalimbali ikiwemo
ujenzi wa madarasa ambapo hadi sasa wamejenga madarasa mawili katika shule ya
sekondari Mwalukwa ambapo kila kaya ilikuwa ikichanga kiasi cha Shilingi elfu
ishirini na moja.
Naye katibu wa Jumuiya
ya wazazi wilaya ya Shinyanga Vijijini Abdalah Kilobi ameitaka jamii
kuhakikisha inawalea watoto katika
maadili yampasayo ili kujenga jamii iliyositarabika
na yenye kuwa na matunda mazuri kwa taifa lijalo.
Nao baadhi ya wachama wa chama cha mapinduzi (CCM) kata ya
Mwalukwa wamepongeza kuadhimisha miaka
44 ya (CCM) kutokana na mabadiliko
makubwa yaliyofanywa na chama hicho hapa nchini ikiwemo ukuaji wa uchumi toka
uchumi wa chini hadi kati, uboresheaji wa miundombinu mbalimbali ikiwemo ujenzi
wa Reli ya Kisasa na upelekaji wa umeme vijijini.
Maadhimisho ya Chama
cha Mapinduzi ufanyika kila mwaka
ifikapo mwezi February tarehe 5.
Wakazi wa Mwalukwa wakiwasikiliza Viongozi wa Jumuiya ya Wazazi Shinyanga Vijijini waliofika kuadhimisha miaka 44 ya (CCM)