Mchungaji wa kanisa la TAG Deliverance Temple lililoko Nyasubi wilayani Kahama, Adrehem Mlelwa akihubiri neno la Mungu kwenye ibada iliyofanyika kanisani hapo jana.
Na Suzy Luhende, Shinyanga
Mchungaji wa kanisa la Tanzania Asemblies of God (TAG) Kahama Deliverence Temple, Adrehem Mlelwa amesema kwa kushirikiana na wazee wa kanisa na waumini wa kanisa hilo wanatarajia kuanza maombi ya siku 90 kuanzia Januari 11, mwaka huu yenye lengo la kuliombea taifa amani.
Akizungumza na mwandishi wa habari hii, mchungaji kiongozi Mlelwa wa kanisa hilo lililoko mtaa wa Nyasubi wilayani Kahama Mkoa wa Shinyanga amesema mbali na kuombea amani, pia maombi hayo ni maalum kwa ajili ya na kuliepusha na magonjwa mbalimbali pamoja na kuombea uchumi wa nchi na wa kila Mtanzania.
Mlelwa amesema mwaka jana kutokana na janga la Corona, uchumi wa baadhi ya taasisi yakiwemo makanisa uliyumba, hivyo katika mwaka huu kanisa hilo linaanza kwa maombi ya siku 90 kwa ajili ya kuliombea taifa amani uchumi wa nchi ukue na kuliepushe na magonjwa mbalimbali yakiwemo ya mlipuko.
Alisema mwaka uliopita wachungaji wengi walishindwa kuhubiri injili kwa kuhofia ugonjwa wa Corona na wachungaji wengi waliishi maisha magumu na wengine kurudi nyuma kiroho, na wengine kukimbia makanisa yao familia zao kwa ajili ya njaa kwa sababu washirika walikuwa hawahudhulii kanisani, hivyo kwa mwaka huu wanasimama imara kuliombea taifa na kumuomba Mungu afungue milango ya baraka na kuepusha magonjwa.
"Tulikuwa tunategemea wageni kutoka nje kwa ajili ya kuhubiri neno la Mungu kufanya semina mbalimbali lakini vyote vilisimama, kwa mwaka huu tunaomba tumaini la nchi lirudi magonjwa ksma hayo yasijirudie tena amani iwepo na watu wote waweze kukuza uchumi wao na kuweza kumtukuza Mungu siku zote," amesema Mlelwa
"Pia changamoto nyingine iliyosababishwa na ugonjwa wa Corona mwaka jana watumishi wengi waliacha uaminifu wa kufundisha mafundisho ya kweli walianza kufundisha mafundisho ya uongo ili waweze kupata chochote kwa mshirika,lakini pia serikali yetu ilikosa amani na uchumi wa ulisimama hivyo mwaka huu tunaanza kwa maombi, ili uchumi wetu uweze kukua kwa haraka amani iwepo na magonjwa ya aina yeyote yashindwe kwa jina la Yesu," amesema Mlelwa.
Mchungaji Mlelwa pia amesema katika maombi hayo watamuombea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Jonh Magufuli ili maono yake makubwa ya kufanya maendeleo ya nchi yaweze kutimia kwa wakati, ikiwa ni pamoja na kumuombea waziri mkuu, mawaziri wa sekta zote wabunge na viogozi wote wanaosimamia maendeleo ya nchi.
Baadhi ya waumini wa kanisa hilo Liberia Shirima na Jacob Kulola wamesema wanaungana na mchungaji katika kufanya maombi ya siku 90 ambayo wanatarajia yatasaidia kuepusha magonjwa yataongeza uchumi, na yataleta amani katika nchi ya Tanzania.
Katika hatua nyingine, Mchungaji Mlelwa aliwataka waumini wa kanisa hilo kuijua ibada ya kweli inayompendeza Mungu ambayo ni ibada ya kujitakasa inayofanyika kati ya mtu na Mungu pekee ambayo inafanyika kwa siri bila kujua mtu mwingine.
"Ili uweze kubarikiwa lazima uziondoe ibada za uongo na unatakiwa uandae sadaka yako kutoka nyumbani kwa sili wala usijue mkono wako wa kushoto, kuwa unasadaka kiasi gani, tusipende kufanya ibada ili tuonekane kwa mtu, tunayakiwa tufanye ibada kwa kumsikiliza Mungu,na sadaka zote ziwe shukrani au zaka ni ibada za siri, hivyo kila mmoja atoe sadaka ya siri ili aweze kubarikiwa," amesema Masihi.
Amesema maombi mengi ya watu waliookoka hayafanikiwi kwa sababu kwa sababu hawafanyi ibada ya sirini, hawatoi sadaka ya sirini wanafanya ibada kwa kujionyesha na wanaenda kanisani kwa kujionyesha hivi na mimi akanione mchungaji nipo kanisani au wakanione nimefanya hiki au nimevaa vizuri hivyo aliwataka wabadilike ili waweze kuzichota baraka kwa wakati.
PICHA
Mchungaji Mlelwa akihubiri kanisani hap
Wazee wa kanisa hilo wakiwa ni sehemu ya misa ya Jumapili
Waumini wa kanisa la TAG Deliverance Temple wakimwabudu Mungu kanisani hapo
Waumini wa kanisa hilo wakiendelea na ibada
Wazee wa kanisa wa kanisa hilo wakitoa divai na mkate kwa ajili ya kushiriki waumini wa kanisa hilo kwa ishara ya kumkumbuka yesu mwana wa Mungu na kujiweka upya mwaka 2021 katika kufanya matendo mema
Waumini wa kanisa la TAG Deliverance Temple kata ya Nyasubi wilayani Kahama wakitoka kanisani baada ya kumaliza ibada ya mchana iliyofanyika kanisani hapo