RC MOROGORO AAMURU KUSWEKWA NDANI WENYEVITI 21


MKUU wa mkoa wa Morogoro, Loata Ole Sanare ameagiza kukamatwa na kuwekwa ndani wenyeviti wa vitongoji 21 wa halimashauri ya mji mdogo wa mikumi wilaya ya Kilosa, kufuatia kutowahamasisha wananchi kushiriki katika ujenzi wa madarasa.

RC Sanare amemvua nyadhifa yake Mwalimu Mkuu wa shule ya sekondari Kauzeni iliyopo Manispaa ya Morogoro Bwana Exavery Makaranga kufuatia kukaa miaka sita kwenye shule hiyo bila maendeleo yoyote.

Awali akitoa taarifa ya ujenzi wa madarasa katika shule ya sekondari mikumi, mtendaji wa mji mdogo mikumi Omary Jaka akatoa changamoto inayokwamisha ujenzi huo, ambapo kufuatia hali hiyo mkuu wa mkoa wa Morogoro Loata Ole Sanare akalazimika kutoa maagizo ya kukamatwa kwa viongozi hao.

RC Sanare amemuagiza Afisa Elimu mkoa wa Morogoro Mhandisi, Joyce Baravuga kumuondoa kwenye nafasi ya mkuu wa shule ya sekondari Kauzeni Bwana Exavery Makaranga kufuatia kushindwa kufanya maendeleo yoyote kwenye shule hiyo.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464