SIMBA SUPER CUP: SIMBA YAANZA KWA USHINDI MNONO


Na Damian Masyenene
Timu ya Soka ya Simba SC ya Jijini Dar es Salaam imeanza vyema katika mashindano maalum ya 'Simba Super Cup' ya kujiandaa na michuano ya Klabu Bingwa Afrika kwa kuibuka na ushindi mnono wa mabao 4 kwa 1 dhidi ya wageni wao, Al Hilal ya nchini Sudan.

Katika mchezo huo uliochezwa saa 11 jioni kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam, mabao ya Wekundu wa Msimbazi yamefungwa na Rally Bwalya, Perfect Chikwende na Bernad Morrison aliyepoachika mawili, huku bao pekee la Al Hilal likifungwa na Salim Mohamed, huku kiungo Rally Bwalya akiibuka nyota wa mchezo huo na kuzawadiwa Sh 500,000.

Michuano hiyo inayozishirikisha klabu bingwa za Simba SC ya Tanzania, Tp Mazembe ya DR Congo na Al Hilal ya Sudan itaendelea tena Ijumaa kwa mchezo wa Al Hilal dhidi ya Tp Mazembe.


Kiungo Rally Bwalya (Kushoto) akikabidhiwa hundi ya Sh 500,000 baada ya kuibuka nyota wa mchezo huo
Kiungo Rally Bwalya akipiga shuti na kufunga bao la kwanza kwa Simba SC
Mchezaji Bernad Morrison akishangilia kwa aina yake baada ya kuifungia Simba SC bao la tatu





Picha zote na Simba SC Tanzania
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464