ASKOFU MACHIMU AZINDUA WIMBO WA TANZANIA YA AMANI WA KWAYA YA DYNAMIC EAGT USHIRIKA SHINYANGA...TAZAMA VIDEO HAPA

Askofu wa Kanisa la EAGT Ushirika Makimbilio Healing Center mjini Shinyanga, Raphael Machimu akionesha DVD ya Wimbo Maalumu wa Picha uliopewa jina la Tanzania ya Amani kutoka Dynamic Choir EAGT Ushirika Shinyanga.

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Askofu wa Kanisa la Evangelistic Assemblies of God Tanzania (EAGT) Ushirika Makimbilio Healing Center mjini Shinyanga, Raphael Machimu amezindua Wimbo Maalumu wa Tanzania ya Amani kutoka Kwaya ya Dynamic ya kanisa la EAGT Ushirika Shinyanga.

Uzinduzi wa wimbo wa Tanzania ya Amani umefanyika leo Jumapili Februari 28,2021 katika kanisa hilo lililopo Ushirika Mjini Shinyanga ambapo pia Askofu Raphael Machimu ameongoza Maombi Maalumu kuombea Amani ya Tanzania pamoja na Kumuomba Mungu aliepushe Taifa na Ugonjwa wa Corona.

Akizindua na kuweka Wakfu CD/DVD ya Wimbo huo, Askofu Machimu amesema wimbo wa Tanzania ya Amani kutoka Dynamic Choir EAGT Ushirika Shinyanga umegusa viongozi wan chi kwa kazi wanayofanya katika kulinda amani ya nchi hivyo kuwaomba Wakisto na watu mbalimbali kununua CD ya wimbo huo ambao pia umewekwa katika Mtandao wa Youtube katika Chaneli ya Dynamic Choir EAGT Ushirika Shinyanga.

“Tunazindua CD hivyo tunapozindua CD hii ni muhimu tuombe kwa ajili ya Rais wetu Mpendwa wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa sababu amekuwa kiongozi wa mfano katika kuimarisha amani ya nchi yetu”,amesema Askofu Machimu.

Askofu Machimu ameeleza kuwa Rais Magufuli ameonesha mfano mkubwa katika kusimamia imani na hasa katika kukabiliana na Ugonjwa hatari wa Corona na amekuwa mhamasishaji mkubwa kwa Watanzania kumtegemea Mungu ili aondoe na kutokomeza ugonjwa wa Corona.

Katika kumuombea Rais Magufuli na viongozi wengine wa kitaifa, Askofu Machimu pia amemuombea Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Zainab Telack, Kamanda wa Polisi mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko kwa jinsi ambavyo amesimamia vyema mkoa wa Shinyanga ambao hapo awali ulikuwa unasifika kwa matukio mabaya ikiwemo mauaji ya vikongwe, watu wenye ualbino n.k

Aidha amesema wimbo wa Tanzania ya Amani ni wimbo mzuri akisema "Hii CD ya wimbo huu ukiwa nayo nyumbani utafurahi,waimbaji wamefanya kazi nzuri. Hii ni kazi takatifu kwa ajili ya kumpa heshima Mungu".

Mwenyekiti wa Kwaya ya Dynamic Daniel Chunga amesema lengo la wimbo huo maalumu wa picha walioupa jina la Tanzania ya Amani ni Kumshukuru Mungu kwa ajili ya kuilinda nchi ya Tanzania na kuliepusha taifa na majanga mbalimbali ikiwemo ugonjwa wa Corona.

“Kupitia wimbo huu tumezalisha nakala 150 zitakazouzwa leo na tutaweka wimbo huu katika Chaneli ya kwaya yetu Youtube”,amesema.

Kwa upande wake, Mgeni wakati wa uzinduzi huo, Mhandisi Edward Mollel amewapongeza wanakwaya kwa kutunga na kuimba wimbo wenye ujumbe mzuri huku akiwasisitiza waimbaji kuendelea kuwa wamoja, kushikamana na kushirikiana.



ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Waimbaji wa Kwaya ya Dynamic ya Kanisa la EAGT Ushirika Makimbilio Healing Center mjini Shinyanga wakiimba wakati wa uzinduzi wa Wimbo Maalumu wa Picha uliopewa jina la Tanzania ya Amani katika kanisa hilo leo Jumapili Februari 28,2021 . Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Waimbaji wa Kwaya ya Dynamic ya Kanisa la EAGT Ushirika Makimbilio Healing Center mjini Shinyanga wakiimba wakati wa uzinduzi wa Wimbo Maalumu wa Picha uliopewa jina la Tanzania ya Amani katika kanisa hilo.
Askofu wa Kanisa la Evangelistic Assemblies of God Tanzania (EAGT) Ushirika Makimbilio Healing Center mjini Shinyanga, Raphael Machimu akiweka Wakfu CD ya Wimbo Maalumu wa Picha uliopewa jina la Tanzania ya Amani katika kanisa hilo leo Jumapili Februari 28,2021
Askofu wa Kanisa la EAGT Ushirika Makimbilio Healing Center mjini Shinyanga, Raphael Machimu akikata utepe kuzindua rasmi wimbo Maalumu wa Picha uliopewa jina la Tanzania ya Amani katika kanisa hilo leo Jumapili Februari 28,2021. Wa kwanza kushoto ni Mweka Hazina wa Kwaya ya Dynamic Veronica Shinyanga akifuatiwa na Mgeni rasmi Mhandisi Edward Mollel. Kulia ni Mwenyekiti wa kwaya ya Dynamic, Daniel Chunga.
Askofu wa Kanisa la Evangelistic Assemblies of God Tanzania (EAGT) Ushirika Makimbilio Healing Center mjini Shinyanga, Raphael Machimu akizungumza baada kuzindua Wimbo Maalumu wa Picha uliopewa jina la Tanzania ya Amani katika kanisa hilo leo Jumapili Februari 28,2021
Askofu wa Kanisa la EAGT Ushirika Makimbilio Healing Center mjini Shinyanga, Raphael Machimu akionesha CD/DVD ya Wimbo Maalumu wa Picha uliopewa jina la Tanzania ya Amani kutoka Dynamic Choir EAGT Ushirika Shinyanga.
Askofu wa Kanisa la EAGT Ushirika Makimbilio Healing Center mjini Shinyanga, Raphael Machimu akionesha CD/DVD ya Wimbo Maalumu wa Picha uliopewa jina la Tanzania ya Amani kutoka Dynamic Choir EAGT Ushirika Shinyanga.
Muonekano wa DVD ya wimbo wa Tanzania ya Amani
Mgeni rasmi Mhandisi Edward Mollel akionesha CD ya wimbo wa Tanzania ya Amani.
Mwenyekiti wa Kwaya ya Dynamic Daniel Chunga akisoma risala kuhus Wimbo wa Tanzania ya Amani ambapo alisema lengo la wimbo huo maalumu wa picha ni Kumshukuru Mungu kwa ajili ya kuilinda nchi ya Tanzania na kuliepusha taifa na majanga mbalimbali ikiwemo ugonjwa wa Corona.
Askofu wa Kanisa la Evangelistic Assemblies of God Tanzania (EAGT) Ushirika Makimbilio Healing Center mjini Shinyanga, Raphael Machimu akiongoza Maombi Maalumu kuombea Amani ya Tanzania pamoja na Kumuomba Mungu aliepushe Taifa na Ugonjwa wa Corona.
Askofu wa Kanisa la Evangelistic Assemblies of God Tanzania (EAGT) Ushirika Makimbilio Healing Center mjini Shinyanga, Raphael Machimu akiongoza Maombi Maalumu kuombea Amani ya Tanzania pamoja na Kumuomba Mungu aliepushe Taifa na Ugonjwa wa Corona.
Maombi Maalumu kuombea Amani ya Tanzania pamoja na Kumuomba Mungu aliepushe Taifa na Ugonjwa wa Corona yakiendelea.

Tazama Video : Dynamic Choir EAGT Ushirika Shinyanga - Tanzania ya Amani


Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464