DROO YA 32 BORA KOMBE LA FA: YANGA VS KENGOLD, SIMBA VS AFRICAN LYON


DROO ya 32 bora (raundi ya nne) michuano ya Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) maarufu kama Kombe la FA imefanyika leo kwa timu 32 kupangiwa michezo ambayo inatarajiwa kupigwa kati ya Februari 27 na 28 mwaka huu kwa ajili ya kupata timu 16 zitakazotinga raundi ya tatu (16 bora) ya michuano hiyo.

Bingwa mtetezi wa michuano hiyo, Simba SC watakuwa wageni wa African Lyon ya Dar es Salaam iliyoko ligi daraja la kwanza Tanzania Bara, huku Yanga SC ikipangiwa kumenyana na Kengold FC ya Chunya mkoani Mbeya, ambapo mchezo huo utapigwa katika dimba la Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

Tazama ratiba kamili hapa
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464