Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, akifungua Kongamano la kimataifa la Uwekezaji katika Sekta ya Madini lenye lengo la kutangaza fursa za Uwekezaji katika Sekta za Madini ziliopo Nchini na kuwaunganisha pamoja Wachimbaji na watoa huduma kwenye Shughuli mbalimbali zinazofanyika Migodini.
Kongamano hilo la siku tatu lenye kauli mbiu "Sekta ya Madini kwa Uchumi Imara na Maendeleo Endelevu" limefunguliwa leo Febuari 22,2021 katika Kituo cha mikutano cha Kimataifa cha Mwalimu Nyerere JNICC Jijini Dar es salaam.
Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan, akiangalia moja ya kifaa kinachotumika kwa Utafiti wa kuweza kujua ubora na uhalisia wa Madini XRF alipotembelea Banda la Tume ya Madini kwenye maonesho ya Shughuli za Madini katika Kongamano la kimataifa la Uwekezaji katika Sekta ya Madini 2021 leo Jijini Dar es salaam. Kushoto ni Waziri wa Madini Mhe. Doto Biteko.
Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan, akiangalia bidhaa mbalimbali za mapambo alipotembelea maonesho ya shughuli za Madini katika Kongamano la kimataifa la Uwekezaji katika Sekta ya Madini 2021 lenye lengo la kutangaza fursa za Uwekezaji katika Sekta za Madini ziliopo nchini na kuwaunganisha pamoja wachimbaji na watoa huduma kwenye shughuli mbalimbali zinazofanyika migodini. Kushoto ni Waziri wa Madini, Doto Biteko.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan (kulia), akikabidhi tuzo kwa Mwakilishi wa Kampuni ya Geita Gold Mine Tanzania, Simon Peter Shayo (katikati) kwa kutambua mchango wa kampuni hiyo na kufanya vizuri katika kutekeleza Sheria zinazosimamia sekta ya Madini na mchango wa mlipa kodi na wadau walioshiriki vizuri kwa Jamii CSR hapa nchini. Kushoto ni Waziri wa Madini, Doto Biteko.
Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan, akiagana na Waziri wa Madini, Doto Biteko baada ya kufungua Kongamano la kimataifa la Uwekezaji katika Sekta ya Madini 2021 katika Kituo cha mikutano cha Kimataifa cha Mwalimu Nyerere JNICC Jijini Dar es salaam leo.
Wadau mbalimbali katika sekta ya madini waliohudhuria kongamano la la kimataifa la Uwekezaji katika Sekta ya Madini 2021 wakimsikiliza Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan (hayupo pichani)
Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais