POLISI Wilaya ya Nachingwea, mkoani Lindi, inamshikilia kwa mahojiano mkazi wa Kitongoji cha Majengo, Ahamadi Makotta (43) kwa tuhuma za kumuua kaka yake, Abdull Makotta (55).
Inadaiwa kuwa mtuhumiwa alifanya mauaji hayo katika ugomvi unaoelezwa kugombea nyumba ya urithi iliyoachwa na marehemu baba yao.
Tukio hilo linadaiwa kufanyika eneo la Majengo, Alhamisi saa 9:40 alasiri.
Kamanda wa Polisi mkoani Lindi, ACP Mtatiro Kitinkwi, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kueleza kuwa mtuhumiwa Ahamadi Makota amekamatwa, na anaendelea kuhojiwa na Jeshi hilo.
Kamanda Kitinkwi alisema watamfikisha mahakamani mtuhumiwa huyo baada ya kukamilika taratibu zikiwamo za upelelezi.
Pia, mewasisitiza wananchi kuacha kujichukulia sheria mikono wanaposhindwa kuelewana, badala yake wawatumie viongozi wakiwamo wazee wa ukoo wanaowazunguka, dini na serikali.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464