MBUNGE KATAMBI ATOA KADI 272 ZA BIMA YA AFYA KWA WATOTO WENYE MAHITAJI MAALUM, CCM YAPONGEZA


Katibu wa Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini (Patrobasi Katambi) Samweli Jackson (kushoto), akimkabidhi Kadi 272 za Bima ya Afya CHF iliyoboreshwa, Katibu wa Itikadi Siasa na Uenezi CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini, Said Bwanga, kwa niaba ya Mbunge huyo, kwa ajili ya kusaidia watoto wenye mahitaji maalum kupata matibabu bure mwaka mzima.

Na Marco Maduhu, Shinyanga
MBUNGE wa Jimbo la Shinyanga Mjini, Patrobasi Katambi (CCM) ambaye pia ni Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira, ametoa kadi za bima ya afya CHF iliyoboreshwa kwa watoto wenye mahitaji maalum, kwa ajili ya kuwa rahisishia upataji wa huduma za matibabu bure na kuimarisha afya zao.

Kadi hizo zilitolewa jana na Katibu wa Mbunge huyo, Samweli Jackson kwenye kilele cha maadhimisho ya miaka 44 ya kuzaliwa kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambayo yalifanyika kwenye kituo cha kulea watoto wenye mahitaji maalum Buhangija kilichopo Ibinzamata manispaa ya Shinyanga.

Jackson akizungumza kwa niaba ya Katambi, amesema Mbunge aliguswa na suala la ukosefu wa matibabu bure kwa watoto wenye mahitaji maalum wakiwamo wenye ualbino, mtindio wa ubongo na yatima, na kuamua kutoa kadi hizo.

Amesema wametoa kadi za bima ya afya CHF iliyoboreshwa 272, katika vituo vitatu vya kulea watoto wenye mahitaji maalum, ambapo katika kituo cha Buhangija kadi 231, kituo cha Kitangili cha watoto wenye mtindio wa ubongo Kadi 21 na kituo cha yatima cha Bushushu kadi 30, ambazo zitawasaidia upataji wa matibabu bure mwaka mzima.

“Mbunge wenu Katambi alifanya ziara kwenye vituo hivi vitatu vya kulea watoto wenye mahitaji maalum, na kuguswa na suala la upataji wa matibabu, na kunituma nizilete kwenu Kadi hizi za Bima ya afya CHF iliyoboreshwa ambazo zitakuwa msaada mkubwa kwenu kwa kupata matibabu bure mwaka mzima,” amesema Jakson.

“Kazi ya Mbunge ni kutumikia wananchi, kitu ambacho ana kifanya Mbunge wenu Patrobas Katambi, na kama Mwananchi ana changamoto yoyote afike kwenye ofisi ya Mbunge, na mimi nitamsikiliza na kisha kumwasilishia Mbunge ili tatizo lake litafutiwe ufumbuzi,”ameongeza.

Naye Mwalimu mlezi wa kituo cha kulea watoto wenye ualbino cha Buhangija Fatuma Jilala, alisema miongoni mwa changamoto kubwa ambayo ilikuwa ikiwakabili ni upataji wa matibabu, na kumshukuru Mbunge Katambi kwa kuwapatia Bima hizo za CHF, ambazo zimeondoa tatizo hilo.

Aidha baadhi ya watoto wenye uhitaji maalum ambao wamepata Kadi za Bima ya afya CHF, akiwamo Seba Bida na Jesca Marco, walisema kadi hizo zitakuwa msaada mkubwa kwao na kuwaondolea tatizo la ukosefu wa matibabu, ambapo kwa sasa watakuwa wakitibiwa bure na kuimarisha afya zao.

Pia Diwani wa Ibinzamata Ezekiel Nsabo, amesema jukumu la kuwalea watoto wenye uhitaji ni la kila mtu, na ndio maana ameamua kuungana na Mbunge Katambi kuwa fariji watoto hao, na kuandaa chakula cha pamoja kula nao wakiwamo na wananchi, ili waguswe na kuwasaidia misaada mbalimbali.

Kwa upande wake Mgeni Rasmi kwenye maadhimisho hayo, Katibu wa Itikadi Siasa na Uenezi wa CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini, Said Bwanga, amempongeza Mbunge Katambi kwa kutekeleza ilani ya chama hicho, kwa kutumikia wananchi wa jimbo lake pamoja na kusaidia watoto wenye mahitaji maalum.

Katika hatua nyingine amewataka wananchi kuendelea kuchukua tahadhari ya kujikinga na maambukizi ya virusi vya Corona, kwa kunawa mikono kwa sabuni na majitiririka, pamoja na kufuata ushauri ambao unatolewa na wataalamu wa afya.

TAZAMA PICHA HAPA CHINI
Katibu wa Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini, (Patrobasi Katambi) Samweli Jacksoni, akizungumza kwa niaba ya mbunge huyo kwenye kilele cha maadhimisho ya sherehe ya miaka 44 ya kuzaliwa kwa Chama cha Mapinduzi CCM.
Katibu wa Itikadi Siasa na uenezi CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini Said Bwanga, akizungumza kwenye sherehe hiyo ya kuzaliwa miaka 44 ya CCM, iliyofanyika katika kituo cha kulea watoto wenye mahitaji maalum Buhangija.
Mwenyekiti wa jumuiya ya umoja wa vijana UVCCM Wilaya ya Shinyanga Mjini Dotto Joshua, akizungumza kwenye Sherehe ya miaka 44 ya CCM. iliyofanyika katika kituo cha kulea watoto wenye mahitaji maalum Buhangija.
Diwani wa Ibinzamata Ezekiel Nsabo, akizungumza kwenye Sherehe ya miaka 44 ya CCM. iliyofanyika katika kituo cha kulea watoto wenye mahitaji maalum Buhangija.
Mtendaji wa Kata ya Ibinzamata Victor Kajuna, akizungumza kwenye Sherehe ya miaka 44 ya CCM. iliyofanyika katika kituo cha kulea watoto wenye mahitaji maalum Buhangija.
Wananchi wakiwa kwenye Sherehe ya miaka 44 ya Chama cha Mapinduzi CCM, iliyofanyika katika kituo cha kulea watoto wenye mahitaji katika kituo cha Buhangija.
Sherehe ikiendelea.
Sherehe ikiendelea.
Sherehe ikiendelea.
Sherehe ikiendelea.
Sherehe ikiendelea.
Sherehe ikiendelea.
Sherehe ikiendelea.
Sherehe ikiendelea.
Meza kuu wakiwa kwenye Sherehe ya miaka 44 ya CCM.
Katibu wa Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini (Patrobasi Katambi) Samweli Jacksoni, kushoto, akimkabidhi Kadi za Bima ya Afya CHF iliyoboreshwa 272, Katibu wa Itikadi siasa na uenezi CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini, Said Bwanga, kwa niaba ya Mbunge huyo kwa ajili ya kusaidia watoto wenye mahitaji maalum, kupata matibabu bure mwaka mzima.
Katibu wa Itikadi siasa na uenezi CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini, Said Bwanga,akigawa Kadi za Bima ya afya CHF iliyoboreshwa kwa watoto wenye mahitaji maalum, ambazo zimetolewa na Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobasi Katambi.
Zoezi la ugawaji Kadi za Bima ya Afya CHF iliyoboreshwa likiendelea kutolewa kwa watoto wenye mahitaji maalum.
Zoezi la ugawaji Kadi za Bima ya Afya CHF iliyoboreshwa likiendelea kutolewa kwa watoto wenye mahitaji maalum.
Picha ya pamoja ikipigwa mara baada ya kumalizika kwa Sherehe ya miaka 44 ya kuzaliwa kwa chama cha Mapinduzi CCM, iliyofanyika katika kituo cha kulea watoto wenye uhitaji Buhangija.

Picha na Marco Maduhu




Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464