
Mjasiriamali Magreth Charles akisherehekea siku ya wapendanao na watoto yatima katika kituo cha Bushushu Orphanages Center (SORC).
Na Mwandishi Wetu
KATIKA kusherehekea siku ya Wapendanao Duniani, Mjasiriamali kijana, Magreth Charles ameungana na watoto yatima wa kituo cha Bushushu katika manispaa ya Shinyanga kwa kusherehekea nao na kuwapa misaada mbalimbali.
Magreth mbali na kujumuika na watoto hao, pia alikabidhi msaada wa chakula ikiwemo mahindi, ndoo mbili za mafuta ya kupikia na kula nao keki ikiwa ni kuonyesha upendo kwao.
Mjasiriamali huyo amesherehekea na watoto hao ikiwa pia ni sehemu ya kusherehekea siku yake ya kuzaliwa.

Magreth Chales (wa nne kulia) akikabidhi ndoo mbili za mafuta ya kupikia kwa watoto yatima wa kituo cha Bushushu

Magreth Charles akikabidhi msaada wa mahindi kwa watoto hao

Magreth akiwasha mshumaa kwa ajili ya kukata keki kusherehekea siku yake ya kuzaliwa.

Akifurahia keki na watoto hao

Akikata keki na watoto hao

Ukataji wa keki ukiendelea

Watoto wakiendelea kukata na kufurahia keki

Magreth Charles akimlisha keki mmoja wa watoto yatima katika kituo cha Bushushu

Magreth Charles akimlisha keki mtoto

watoto wakiendelea kula keki

Rafiki wa Magreth akimlisha mtoto keki

rafiki wa Magreth akimlisha keki mtoto

Magreth Charles pamoja na marafiki zake wakifurahia na kula matunda na watoto yatima wa kituo cha Bushushu

Magreth Charles akiwa katika picha ya pamoja na watoto hao

