NAIBU DPP BW. EDSON MAKALLO AWATAKA WATUMISHI WA MASHTAKA KUZINGATIA MAADILI YA UTUMISHI KWENYE MAENEO YAO

Naibu Mkurugenzi wa Mashtaka Bw. Edson Makallo akifungua mafunzo ya Ukusanyaji, Uchakataji, Utumaji na Utunzaji wa Takwimu  za Kesi za Jinai na Kumbukumbu za Makosa ya Rushwa kwa Makatibu Sheria yanayofanyika mkoani Singida kuanzia tarehe 3 Februari,2021 hadi tarehe 08 Febry,2021. Kushoto kwa Bw. Makallo ni  Mkurugenzi Msaidizi Sehemu ya Uratibu wa Upelelezi Bi. Neema Mwanda.

NA MWADISHI Ofisi ya Taifa ya Mashtaka.

Naibu Mkurugenzi wa Mashtaka Bw. Edson Makallo akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa mafunzo ya Ukusanyaji, Uchakataji,Utumaji na Utunzaji wa Takwimu za Kesi za Jinai na Kumbukumbu za Makosa ya Rushwa kwa Makatibu Sheria yanayofanyika Mkoani Singida kuanzia leo tarehe 3 Februari 2021 hadi 08 Februari,2021. Kushoto ni Mkurugenzi wa Raslimali Watu wa Ofisi ya  Taifa ya Mashtaka Bw. Sheusi Mburi pamoja na viongozi wengine kutoka Ofisi ya Taifa ya Mashtaka.

Naibu Mkurugenzi wa Mashtaka Bw. Edson Makallo  amewasihi watumishi wa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka kuzingatia Maadili katika maeneo yao ya kazi pamoja na kufanya kazi kwa bidii.

Naibu Mkurugenzi Makallo ameyasema hayo mapema leo wakati akifungua mafunzo ya ukusanyaji, uchakataji, utumiaji na utunzaji wa takwimu za kesi za Jinai na kumbukumbu  za makosa ya Rushwa kwa Makatibu Sheria wa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka yanayofanyika Mkoani Singida kuanzia tarehe 03 Februari 2021.hadi tarehe 08  Februari,2021

Bw. Makallo amesema kada ya utumishi wa Makatibu wa  Sheria inakumbana na changamoto mbalimbali za kiutendaji na kimaadili  hivyo mafunzo hayo wanayopatiwa yatumike kuwasaidia na kuboresha utendaji wao wa kazi.

Amesema katika miaka ya karibuni dunia imeshuhudia kuwepo kwa mabadiliko makubwa katika nyanja mbalimbali za maisha ya mwanadamu kiuchumi,kijamii, kisiasa, kiteknolojia na kiutamaduni ambapo athari za mabadiliko  hayo ni pamoja na kubadilika kwa mbinu za kupanga na kutekeleza uhalifu na hivyo kuwataka Makatibu wa Sheria wakiwa ni miongoni mwa watoa huduma katika taasisi ya Haki Jinai kukumbuka kuwa wana jukumu kubwa la kuhakikisha wanashiriki katika kupambana na kuzuia uhalifu huo kwa njia ya kutekeleza vema majukumu yao.

Aidha, amesema kuwa  Ofisi ya Taifa ya Mashtaka imejipanga vyema katika kushughulikia matendo ya mmomonyoko wa maadili kwa watumishi wa Umma ambapo hatua madhubuti zimekuwa zikichukuliwa kwa watumishi wanaobainika kujihusisha na vitendo vya utovu wa nidhamu.

Amesema watumishi wa Umma wakizingatia miiko iliyopo katika utendaji wao wa kila siku huleta matokeo chanya kwa huduma wanazotoa kwa jamii na hivyo jamiu hujenga imani kwa serikali na kuleta hali ya Usalama.

Bw. Makallo alitoa rai kwa Makatibu Sheria waliohudhuria mafunzo hayo  kuwa kila aliyepata mafunzo arudipo katika sehemu yake ya kazi  kuweka ujuzi aliopata kwa vitendo na kushirikisha ujuzi walioupata kwa wengine  ambao hawajapata nafasi ya kuhudhuria mafunzo ili kupanua ushiriki wa mafunzo wa Makatibu Sheria wengi zaidi.

Aidha, amesisitiza umuhimu wa kutunza siri zinazohusu taarifa za majalada yanayowafikia  huku wakielewa kwamba suala la utunzaji wa siri ni la lazima kwa watumishi wote wa Umma.

Mafunzo hayo ya siku sita kwa Makatibu Sheria  yameandaliwa kwa ushirikiano wa Divisheni ya Usimamizi wa Kesi na Uratibu wa Upelelezi  na  Divisheni ya Makosa ya Udanganyifu, Utakatishaji Fedha na Rushwa  Ofisi ya Taifa ya Mashtaka.

Katika mafunzo hayo mada mbalimbali  zitatolewa zikiwepo mada juu ya Maadili ya Makatibu Sheria, Kutunza na kushughulikia  majalada ya rushwa, ukusanyaji, uchakataji na utumaji wa takwimu za kesi, utunzaji na mfumo wa regista ya ofisi,mfumo wa kielektroniki wa upokeaji na utunzaji wa majalada, utunzaji wa kumbukumbu na  nyaraka za serikali pamoja na.masuala mengine yanayohusu maadili.

Mkurugenzi Msaidizi Sehemu ya  Usimamizi wa Kesi za Jinai   Bw. Tumaini Kweka akizungumza  katika mafunzo ya ukusanyaji, uchakataji na utumiaji wa takwimu na kumbukumbu za makosa ya rushwa kwa Makatibu Sheria yanayofanyika Mkoa wa Singida kuanzia leo tarehe 3 Februari, 2021 na kumalizika tarehe 08 Februari,2021.Katibu Sheria Ofisi ya Taifa ya Mashtaka  Mkoa wa Dar es Salaam Bi. Gilley Manara akitoa taarifa ya majukumu ya kiofisi katika mafunzo ya ukusanyaji, uchakataji na utumiaji wa takwimu na kumbukumbu za makosa ya rushwa yanayofanyika Mkoani Singida kuanzia tarehe 3 Februari, 2021 na kumalizika tarehe 8 Februari, 2021.

Mkurugenzi Rasilimali Watu Ofisi ya Taifa ya Mashtaka Bw. Seushi Mburi akitoa mada juu ya maadili ya utendaji kazi katika utumishi wa umma na mfumo wa kazi wa mapitio na tathmini ya utendaji kazi  kwa Makatibu Sheria ambao wameudhuria mafunzo ya ukusanyaji, uchakataji na utumiaji wa takwimu na kumbukumbu za makosa ya rushwa yanayofanyika Mkoani Singida kuanzia tarehe 3 Februari, 2021 na kumalizika tarehe 8 Februari, 2021.

Naibu Mkurugenzi wa Mashtaka Bw. Edson Makallo akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa mafunzo ya Ukusanyaji, Uchakataji,Utumaji na Utunzaji wa Takwimu za Kesi za Jinai na Kumbukumbu za Makosa ya Rushwa kwa Makatibu Sheria yanayofanyika mkoani Singida kuanzia tarehe 3 Februari 2021 hadi 08 Februari,2021. Kushoto kwa Bw. Makallo.ni Mkurugenzi wa Raslimali Watu wa Ofisi ya  Taifa ya Mashtaka Been. Sheusi Mburi pamoja na viongozi wengine kutoka Ofisi ya Taifa ya Mashtaka

Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464