Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) Maalim Seif Sharif Hamad (77) ambaye ni Mwenyekiti wa Chama cha ACT- Wazalendo amefariki dunia leo Jumatano Februari 17, 2021 saa 5:26 asubuhi.
Akihutubia Taifa kwa njia ya televisheni, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Mwinyi, amesema Maalim Seif alifariki dunia akiwa katika Taasisi ya Magonjwa ya Moyo ya Jakaya Kikwete iliyopo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) alikokuwa amelazwa tangu Februari 9, 2021.
Rais wa Zanzibar Dk. Hussein Mwinyi ametangaza siku saba za maombolezo kufuatia kifo cha Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad.
''Majira ya saa tano na dakika 26 asubuhi Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad alifariki dunia, Maalim amefariki wakati akiendelea na matibabu katika Hospitali ya Muhimbili ambapo alikuwa amelazwa tangu tarehe 9 mwezi Februari mwaka huu'', amesema Rais Mwinyi.
Rais Mwinyi amesema taifa limepoteza kiongozi mzalendo na shupavu na ametangaza siku saba za maombolezo ambapo bendera zitapepea nusu mlingoti.
Rais Mwinyi amesema taarifa zaidi kuhusu msiba na maziko yake zitaendelea kutolewa na serikali, kwa ushirikiano wa karibu na familia na Chama cha ACT- Wazalendo.