Kaimu Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Shinyanga, Agness Bashemu akizungumza na wananchi wa kata ya Kolandoto (hawapo pichani) katika zoezi la upandaji miti kwenye shule ya sekondari Kolandoto.
Na Mwandishi Wetu, Shinyanga
Viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ngazi ya vijiji na Kata mkoani Shinyanga wametakiwa kujenga utamaduni wa kufatilia ujenzi wa miradi ya maendeleo inayo tekelezwa kwa fedha za serikali na wadau mbalimbali mkoani humo.
Rai hiyo imetolewa na Kaimu Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Shinyanga, Aginess Bashemu wakati akizungumza na wanachama pamoja na wananchi katika hafla fupi ya zoEzi la upandaji miti katika Shule ya Sekondari Kolandoto iliyopo Manispaa ya Shinyanga ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya wiki ya wazazi.
Aidha Bashemu amesema kuwa kuanzia Februari 2, mwaka huu watafanya ziara ya kukagua na kutembelea miradi ya maendeleo inayo tekelezwa katika maeneo mbalimbali ikiwemo ujenzi wa vyumba vya madarasa na miradi mingine.
Kwa upande wao baadhi ya wanachama wa CCM pamoja na Wananchi walioshiriki katika ujenzi wa miradi ya maendeleo wameahidi kuzingatia maelekezo yaliyo tolewa na katibu wachama hicho ngazi ya mkoa hali itakayo saidia kucho chea maendeleo katika maeneo yao.
Hata hivyo, Bashemu ameongoza zoezi la upandaji miti katika Shule ya Sekondari Kolandoto kusaidia kuboresha mazingira ya Shule hiyo pamoja na kuufanya mkoa kuwa na rangi ya kijani.
Katika zoezi hilo, Bashemu alimuagiza mkuu wa Shule ya Sekondari Kolandoto kuainisha mazingira rafiki ya kupanda miti hali itakayo saidia kuepusha uharibifu wa miti inayo pandwa na kisha kuharibiwa wakati wa shughuli mbalimbali za ujenzi shuleni hapo.
Kaimu Katibu wa CCM Mkoa wa Shinyanga, Agness Bashemu akinawa mikono baada ya kupanda mti katika shule ya Sekondari Kolandoto mjini Shinyanga
Baadhi ya viongozi mbalimbali wa chama hicho waliohudhuria zoezi la upandaji miti katika Shule ya Sekondari Kolandoto
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464