WATENDAJI WA VIJIJI NA KATA KISHAPU WATAKIWA KUWEKA WAZI TAARIFA ZA MAPATO NA MATUMIZI

Mkuu wa Wilaya ya Kishapu, Nyabaganga Talaba akizungumza na Madiwani, Wenyeviti wa vijiji, pamoja na wajumbe wa kamati za PETS (ufuatiliaji wa matumizi ya rasilimali za umma) katika kikao cha kufanya maamuzi na kujadili mafanikio na changamoto zilizopo, katika kikao kilichofanyika jana kwenye Ukumbi wa halmashauri wilayani Kishapu

Na Mwandishi Wetu, Kishapu
MAAFISA Watendaji wa Vijiji na Kata wilayani Kishapu  Mkoa wa Shinyanga wametakiwa kutimiza matakwa ya kisheria ya kusoma taarifa ya mapato na matumizi kwa wananchi wilayani humo

Wito huo umetolewa jana na Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) wilaya ya Kishapu, Kidula Masalu wakati akizungumza na Madiwani, Wenyeviti wa vijiji, pamoja na wajumbe wa kamati za PETS (ufuatiliaji wa matumizi ya rasilimali za umma) katika kikao cha kufanya maamuzi na kujadili mafanikio na changamoto zilizo patikana kutokana na taarifa za PETS baada ya wajumbe kuwakilisha taarifa zao katika kikao hicho.

Masalu amesema kuwa ni kosa kisheria viongozi wa kata kushindwa kutoa taarifa za mapato na matumizi ya miradi inayo endelea kwenye maeneo yao na kuwataka madiwani pamoja na wajumbe wakamati za PETS kutoa taarifa Takukuru pindi wanapo baini uwepo wa vitendo vya rushwa kwenye maeneo yao

Hata hivyo, Mkuu huyo wa Takukuru amebainisha kuwa taasisi hiyo imejipanga kusimamia nidhamu ya watumishi katika usimamizi matumizi ya rasilimali za umma.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kishapu, Nyabaganga Talaba amelishukuru shirika la TCRS (Tanganyika Christian Refugee services) la wilayani humo kwa kuwajengea uwezo wa kusimamia matumizi ya rasilimali za umma wananchi, huku akiliomba shilika hilo kuangalia namna ya kuongeza bajeti ya kuwawezesha wajumbe wengine ili waweze kufanya ufatiliaji katika miradi yote inayotekelezwa wilayani humo.

Naye Afisa Miradi wa Shirika la TCRS wilaya ya Kishapu, Mwanamina Jumanne amesema kuwa wao kama viongozi wa shirika kwa kushirikiana na wadau wengine waliamua kutekeleza mradi wa kuwajengea uelewa wananchi juu ya usimamizi wa rasilimali za umma ili kuunga mkono jitihada za serikali katika kudhibiti matumizi mabaya ya rasilimali za umma katika wilaya hiyo, mradi ambao ulianza mwaka 2019 ambapo mpaka sasa wamefanikiwa kusimamia miradi ya utekelezaji wa maji kwa asilimia 100.
Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) wilaya ya Kishapu, Kidula
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, William Jijimya akizungumza katika kikao hicho

Baadhi ya Madiwani, Wenyeviti wa vijiji na wajumbe wa kamati za PETS wakifuatilia kikao hicho




Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464