DC MBONEKO AFANYA ZIARA KWENYE KIWANDA CHA CHAKI 'SHINYANGA STANDARD CHALK'


Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akiwa amebeba maboksi ya chaki za Kiwanda cha Shinyanga Standard Chalk kilichopo katika mtaa wa Miti Mirefu Mjini Shinyanga. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko ametembelea Kiwanda cha Kutengeneza Chaki cha ‘Shinyanga Standard Chalk’kilichopo Mjini Shinyanga na kujionea jinsi uzalishaji wa chaki unavyofanyika na kutoa agizo kwa Wakuu wa Shule katika wilaya hiyo kununua chaki hizo.

Mboneko amefanya ziara katika kiwanda cha Shinyanga Standard Chalk kilichopo katika mtaa wa Miti Mirefu Mjini Shinyanga leo Jumatatu Machi 2,2021.

Akizungumza kiwandani hapo, Mboneko amewapongeza vijana walioanzisha kiwanda hicho kwa kutengeneza chaki mzuri na bora na kutoa agizo kwa Wakuu wa shule zilizopo katika wilaya ya Shinyanga na kuahidi kutafuta masoko zaidi kwenye wilaya zingine.

“Natoa agizo kwa wakuu wa shule zote watumie chaki zinazozalishwa katika kiwanda chetu cha Shinyanga, kuna chaki za kutosha nataka chaki hizi zinunuliwe. Hatuwezi kununua chaki nje ya Shinyanga wakati tunazo hapa kwetu kwenye kiwanda chetu,tena ni chaki nzuri sana na wazalishaji wanafuata taratibu zote za uzalishaji”,amesema Mboneko.

“Nataka kila shule inunue Boksi moja hadi mawili. Mzigo upo wa kutosha na vijana hawa wapo tayari kuwasambazia chaki hadi kwenye shule zenu”,ameongeza Mboneko.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kikundi cha Vijana walioanzisha Kiwanda cha Shinyanga Standard Chalk, Hashim Issa Hashim amesema walianza uzalishaji wa chaki mwezi Aprili 2020 na sasa wana uwezo wa kuzalisha katoni 102 kwa siku.

Amesema licha ya uzalishaji mkubwa wanaofanya bado changamoto kubwa ni ukosefu wa masoko kutokana na soko la ndani kusuasua akibainisha kuwa endapo soko la ndani likiwa zuri basi wataweza kuuza chaki hizo nje ya wilaya ya Shinyanga ambapo amemshukuru Mkuu wa wilaya hiyo, Jasinta Mboneko kuwaunga mkono kwa kuhamasisha wakuu wa shule kununua chaki katika kiwanda hicho.

Hashim amewaomba wenye uhitaji wa Chaki nzuri zenye ubora wa hali ya juu za Kiwanda cha Shinyanga Standard Chalk wafike katika kiwanda hicho kilichopo mtaa wa Miti Mrefu karibu na Ofisi za Ally's Bus  Mjini Shinyanga au wapige simu namba  0713 332 609 au 0747 844 341 au Email shystandard1@gmail.com


Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko (kushoto) akiangalia chaki muda mfupi baada ya chaki hizo kutolewa katika mitambo ya uzalishaji katika Kiwanda cha Shinyanga Standard Chalk kilichopo katika mtaa wa Miti Mirefu Mjini Shinyanga leo Jumanne Machi 2,2021. Katikati ni Mwenyekiti wa Kiwanda cha Shinyanga Standard Chalk, Hashim Issa, kulia ni Mhandisi mkuu wa kiwanda hicho Amani Daniel. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko (kushoto) akiangalia namna uzalishaji wa chaki unavyofanyika katika Kiwanda cha Shinyanga Standard Chalk kilichopo katika mtaa wa Miti Mirefu Mjini Shinyanga
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko (kushoto) akiangalia namna uzalishaji unavyofanyika katika Kiwanda cha Shinyanga Standard Chalk kilichopo katika mtaa wa Miti Mirefu Mjini Shinyanga
Wa pili kushoto ni Mwenyekiti wa Kiwanda cha Shinyanga Standard Chalk Hassim Issa akimwelezea Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko (kushoto) kuhusu uzalishaji wa chaki kwenye Kiwanda cha Shinyanga Standard Chalk kilichopo katika mtaa wa Miti Mirefu Mjini Shinyanga
Muonekano wa sehemu ya mitambo katika Kiwanda cha Shinyanga Standard Chalk kilichopo katika mtaa wa Miti Mirefu Mjini Shinyanga
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko (kushoto) akiangalia namna uzalishaji wa chaki unavyofanyika kwenye Kiwanda cha Shinyanga Standard Chalk kilichopo katika mtaa wa Miti Mirefu Mjini Shinyanga
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko (kushoto) akiangalia chaki zilizoanikwa juani muda mfupi baada ya chaki hizo kutolewa katika mitambo ya uzalishaji katika Kiwanda cha Shinyanga Standard Chalk kilichopo katika mtaa wa Miti Mirefu Mjini Shinyanga
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko (kushoto) akiangalia chaki zilizoanikwa juani muda mfupi baada ya chaki hizo kutolewa katika mitambo ya uzalishaji katika Kiwanda cha Shinyanga Standard Chalk kilichopo katika mtaa wa Miti Mirefu Mjini Shinyanga
Muonekano wa chaki zikiwa zimeanikwa juani
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko (kulia) akiangalia Boksi la kuhifadhia chaki katika Kiwanda cha Shinyanga Standard Chalk kilichopo katika mtaa wa Miti Mirefu Mjini Shinyanga
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko (kushoto) akizungumza katika Kiwanda cha Shinyanga Standard Chalk kilichopo katika mtaa wa Miti Mirefu Mjini Shinyanga
Mwenyekiti wa Kiwanda cha Shinyanga Standard Chalk, Hashim Issa akimwelezea Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko (kushoto) changamoto wanazokutana nazo wakati wa uzalishaji wa chaki ikiwa ni pamoja na kukosa masoko
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko (wa pili kushoto) akizungumza katika Stoo ya kuhifadhia chaki kwenye Kiwanda cha Shinyanga Standard Chalk kilichopo katika mtaa wa Miti Mirefu Mjini Shinyanga
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko (kushoto) akizungumza katika Kiwanda cha Shinyanga Standard Chalk kilichopo katika mtaa wa Miti Mirefu Mjini Shinyanga
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akizungumza katika Kiwanda cha Shinyanga Standard Chalk kilichopo katika mtaa wa Miti Mirefu Mjini Shinyanga
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akiangalia maboksi ya ndani ya chumba cha kuhifadhia chaki katika Kiwanda cha Shinyanga Standard Chalk kilichopo katika mtaa wa Miti Mirefu Mjini Shinyanga
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko (katikati) kulia ni Mwenyekiti wa Kiwanda cha Shinyanga Standard Chalk, Hashim Issa, kushoto ni Mhandisi mkuu wa kiwanda hicho Amani Daniel wakiwa wameshikilia maboksi ya chaki za Kiwanda cha Shinyanga Standard Chalk
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko (katikati) na viongozi mbalimbali wakiwa wameshikilia maboksi ya chaki
Muonekano wa maboksi yenye chaki za Kiwanda cha Shinyanga Standard Chalk
Muonekano wa maboksi ya chaki za Kiwanda cha Shinyanga Standard Chalk


Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog


Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464