Juma Mwambusi
SIKU chache baada ya uongozi wa klabu ya Yanga kulifukuza kazi benchi la ufundi likiongozwa na Kocha Mkuu, Cedric Kaze na msaidizi wake, Nizar Khalfan, Mwenyekiti wa klabu hiyo, Dk. Mshndo Msolla amemtangaza Juma Mwambusi kama kocha wa muda wakati jitihada za kumpata kocha mkuu mpya zikiendelea.
Mwambusi ametajwa kuwa kocha wa muda zikiwa ni wiki kadhaa baada ya kujiondoa klabuni hapo kama kocha msaidizi ili kupata maptibabu kutokana na matatizo ya kiafya yaliyokuwa yakimkabili.
Akitangaza uamuzi wa kumrejesha Mwambusi, Mwenyekiti wa Klabu ya Yanga, Dk. Mshindo Msolla amenukuliwa akisema “Mwambusi ataichukua timu kwasasa wakati tunamtafuta mwalimu mwingine, na kwa bahati nzuri Mwambusi aliondoka na kuaga vizuri, na klabu ilimsaidia kupata matibabu wakati anaumwa na tokea ligi inaanza tulikuwa naye hivyo sio kwamba ana ugeni na timu”
Mwambusi amewahi kuvinoa vilabu vya Mbeya City, Yanga, Singida United na Azam.