Meneja wa Kanda ya Magharibi kutoka benki ya NMB, Sospeter Magese akizungumza na baadhi ya wananchi kwenye uzinduzi wa kampeni maalumu iliyofanyika katika stendi kuu ya mabasi wilayani Kahama iliyokwenda kwa jina la 'Bonge la mpango' itakayoendeshwa kwa kipindi cha miezi mitatu
Na Neema Sawaka, Kahama
WANANCHI wilayani Kahama mkoa wa Shinyanga wametakiwa kuhifadhi fedha zao kwenye taasisi za kifedha ili waweze kujipatia faida itakayowawezesha kujinyanyua kiuchumi kutokana na mashindano mbalimbali ambayo yamekuwa yakianzishwa.
Hayo yalisemwa leo na Meneja wa Kanda ya Magharibi kutoka benki ya NMB, Sospeter Magese kwenye uzinduzi wa kampeni maalumu iliyofanyika kwenye stendi kuu ya mabasi wilayani Kahama iliyokwenda kwa jina la 'Bonge la mpango' itakayoendeshwa kwa kipindi cha miezi mitatu.
Magese amesema kuwa wafanyabiashara wanatakiwa kutumia taasisi za fedha kuhifadhi fedha zao eneo ambalo ni salama kwa kuweza na kujiongezea kipato kupitia mashindano yanayoanzishwa yenye tija.
“Kampeni hii itakuwa ni kanda ya magharibi inayojumuisha mikoa minne ambayo ni Tabora,Simiyu,Kigoma na Shinyanga na imelenga kuhamasisha wateja na wasio wateja kufungua akaunti nakujishindia gari, pikipiki ya mizigo yenye miguu mitatu na fedha taslimu,” amesema Magese.
Magese ameeleza kuwa katika kampeni hiyo maalum yenye lengo la kurejesha faida kwa wateja nakuhamasisha utamaduni wa kujiwekea akiba kwa wananchi ambapo imeanza rasmi jana na kiasi cha Sh. millioni 550 kimetengwa kuendesha zoezi hilo kipindi cha miezi mitatu.
Aidha Magese alisema kuwa zawadi zitatolewa kila wiki kwa washindi pia katika kipindi hiki cha mavuno Benki ya NMB imetoa elimu kwa wananchi kuhakikisha wanahifadhi fedha
Meneja NMB Kanda ya Magharibi, Sospeter Njile Magese (aliyeshika bendera) akiwa na wafanyakazi wa benki hiyo Kanda ya Magharibi na tawi la Kahama wakizindua kampeni ya Bonge la Mpango katika Stendi ku ya Mabasi Kahama Mkoani Shinyanga
Meneja NMB Kanda ya Magharibi, Sospeter Njile Magese akionyesha moja ya zawadi ya pikipiki ya miguu mitatu itakayotolewa kwa washindi katika kampeni ya Bonge la Mpango
Wafanyakazi wa Benki ya NMB Kanda ya Magharibi na tawi la Kahama wakifanya uhamasishaji katika kampeni iliyozinduliwa ya Bonge la Mpango, leo katika stendi kuu ya mabasi mjini Kahama.