


Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan ameapishwa kuwa Rais wa sita wa Tanzania na Jaji Ibrahim Juma katika Ikulu ya Jijini Dar es Salaam.
Hafla ya kuapishwa kwake imefanyika Ikulu Dar es Salaam na kuweka historia ya kuwa Rais wa kwanza mwanamke nchini Tanzania.
Samia amechukua nafasi ya aliyekuwa rais wa Tanzania, John Magufuli aliyefariki dunia Machi 17, 2021 kwa maradhi ya moyo katika hospitali ya Mzena jijini Dar es salaam alikokuwa akipatiwa matibabu.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464