TUGHE SHINYANGA WATOA MISAADA VITUO VYA WATU WENYE MAHITAJI BUHANGIJA NA KOLANDOTO

Mmoja wa wajumbe wa Tughe mkoa wa Shinyanga akigawa vinywaji kwa watoto wenye ulabino na wenye mahitaji katika shule ya Buhangija mjini Shinyanga ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha siku ya Wanawake Duniani

Na Mwandishi Wetu, Shinyanga
WANAWAKE kutoka Chama cha Wafanyakazi wa Serikali na Afya (TUGHE) mkoani Shinyanga jana kiliungana na Watanzania wengine kuadhimisha siku ya Wanawake Duniani kwa kutembelea vituo vya watoto wenye mahitaji pamoja na kituo cha wazee wasiojiweza cha Kolandoto vilivyopo mjini Shinyanga.

Mwenyekiti wa Tughe mkoa wa Shinyanga, Flora Magubo alisema lengo la kutembelea vituo hivyo ni kuwafariji na kutoa misaada ya kibinadamu kama sehemu ya kusherehekea sikukuu hiyo ya wanawake duniani.

Kwa upande wake Mwalimu Mkuu wa Shule ya Buhangija mchanganyiko yenye idadi kubwa ya watoto wenye Ualbino, Fatuma Hamis ameshukuru kwa kupata misaada hiyo.

Nao wazee wanaoishi katika kituo cha Kolandoto akiwemo Juakali Mihangwa wameshukuru Tughe Shinyanga kuwakumbuka na kuwaomba wadau wengine kuwasaidia mahitaji mbalimbali, huku Mlezi wa Kituo hicho, Sophia Kang'ombe akipongeza hatua hiyo na kueleza kuwa bado mahitaji ni mengi kwa wazee hao, hivyo wadau waendelee kuwakumbuka na kuwasaidia ili kukabiliana na baadhi ya changamoto zilizopo..
Mwenyekiti wa TUGHE Shinyanga, Flora Magubo akizungumza baada ya kutembelea vituo vya watu wenye mahitaji maalum Buhangija na Kolandoto
Mjumbe Kamati Tendaji ya Tughe mkoa wa Shinyanga, Experansia Misalaba
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Buhangija mchanganyiko yenye idadi kubwa ya watoto wenye Ualbino, Fatuma Hamis akizungumza baada ya kupokea misaada mbalimbali kutoka Tughe shuleni hapo
Baadhi ya wafanyakazi wa Tughe mkoa wa Shinyanga wakiendelea kugawa zawadi misaada mbalimbali kwa watoto katika shule ya Buhangija

Baadhi ya vitu vilivyotolewa na Wanawake wafanyakazi wa Tughe mkoa wa Shinyanga kwenye kituo cha Wazee Kolandoto na wenye ualbino Buhangija


Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464