Aliyekuwa Mkurugenzi wa SHUWASA, Flaviana Kifizi, enzi za uhai wake
Na Damian Masyenene, Shinyanga
Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira mjini Shinyanga (SHUWASA),Flaviana Kifizi amefariki dunia leo alfajiri Jumanne Aprili 20, 2021 wakati akiendelea kupatiwa matibabu katika hospitali ya taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam baada ya kuugua muda mrefu.
Taarifa kutoka Shuwasa
Kufuatia taarifa za msiba huo, wadau mbalimbali wa maendeleo na waliofanya kazi mbalimbali za utekelezaji wa miradi ya maji mkoani Shinyanga wametoa pole kwa Shuwasa.
Aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Shinyanga, Azza Hilal (CCM), ameandika "Pumzika kwa Amani Dada Flaviana; Mpole, mcheshi, mnyenyekevu, anayeipenda kazi yake, hakika uliitendea haki nafasi yako. Pole kwa familia yake, poleni sana Shuwasa,".
Naye Mwenyekiti wa Chadema mkoa wa Shinyanga, Emmanuel Ntobi ametoa pole zake na kumuelezea Marehemu Flaviana kwa namna alivyoibadilisha Shuwasa na jinsi walivyoshirikiana kwenye kazi wakati Ntobi akiwa Diwani wa Kata ya Ngokolo (2015-2020).
"Flaviana alikuwa mwalimu na Rafiki kwa watu wengi na alikuwa mkarimu kwa watu wote, alikuwa Rafiki aliyejaaliwa kipawa, tutamkumbuka,".
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Lulekia, Ansila Benedict, ameandika "Ni masikitiko makubwa. Mwenyezi Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi. Tutamkumbuka daima kwa uwajibikaji wake uliotukuka,".
MarehemuFlaviana Kifizi (mbele) wakati akitekeleza majukumu yake
MarehemuFlaviana Kifizi (kushoto) wakati akitekeleza majukumu yake
Flaviana Kifizi enzi za uhai wake
Flaviana Kifizzi enzi za uhai wake
Flaviana Kifizi (kulia) akimkabidhi msaada wa ndoo, Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Jasinta Mboneko (kushoto), kwenye utekelezaji wa majukumu yake enzi za uhai wake.
Flaviana Kifizi (wa pili kushoto) Enzi za uhai wake
Marehemu Flaviana akiwa kwenye majukumu yake katika kuhakikisha anasogeza huduma ya maji safi karibu na wananchi