Rais wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Samia Suluhu Hassan
Rais Samia Suluhu Hassan amechaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa kupata kura zote1,862, sawa na asilimia 100 ya kura zote 1,862.
Wajumbe wote waliokuwa ukumbini – 1,876
Walipoiga kura – 1,862
Kura zilizoharibika – 0
Kura za ndio – 1,862 (100%).
Uzoefu wa miaka 34 wa kuwa Mwanachama wa CCM na uzoefu wa miaka 44 akiwa mtumishi wa Serikali vimetosha kumfanya kuwa mwanamke wa kwanza mwenye sifa na uwezo wa kukiongoza chama hicho Taifa.
Uwezo wake aliouonesha wa kufanya kazi kama Makamu wa Rais chini ya Dkt. John Magufuli na hatimaye kuwa Rais wa Tanzania baada ya kifo cha Magufuli vimemfanya aaminiwe kwamba anatosha kuwa Mwenyekiti wa chama hicho kinachotawala.
Lazaro Nyalandu
ALIYEWAHI kuwa mwanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Waziri wa Maliasili na Utalii na kisha baadaye kujiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Lazaro Nyalandu ametangaza rasmi kuondoka Chadema kurejea CCM mbele ya Rais wa Tanzania na Mwenyekiti wa CCM Taifa, Samia Suluhu.
Nyalandu ambaye amekuwa Mwenyekiti wa CHADEMA Kanda ya Kati ametangaza uamuzi huo leo Aprili 30, 2021, kupitia Mkutano Mkuu Maalum wa CCM uliofanyika katika Ukumbi wa Jakaya Kikwete, jijini Dodoma akisema ameamua kurejea nyumbani.
Nyalandu alitangaza kujiondoa CCM mwaka 2017, aliwania kwenye kinyang’anyiro cha kuteuliwa kugombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika uchaguzi Mkuu wa mwaka jana 2020 lakini chama hicho kilimpitisha tundu Lissu kupeperusha bendera ya Chadema hivyo Nyalandu alishindwa licha ya maandalizi ya mapema.
”Mhe Mwenyekiti nakushukuru sana kwa kukubali kunipokea, kukubali kunisamehe na kuniruhusu mimi Lazaro Samwel Nyalandu, kurejea tena nyumbuni, kwa hakika hakuna furaha izidiyo furaha ya mtoto arejeaye nyumbani” amesema Nyalandu.