Mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Jasinta Mboneko (aliyetangulia mbele) akikagua ujenzi wa Zahanati ya kijiji cha Nyaligongo inayojengwa kwa nguvu za wananchi ambao ni wachimbaji wa madini.
Na Marco Maduhu, Shinyanga
WAKAZI wa Kijiji cha Nyaligongo Kata ya Mwakitolyo wilayani Shinyanga ambao wanajishughulisha na uchimbaji wa madini ya Dhahabu, wamejitolea kuanza ujenzi wa Zahanati ambayo itawaondolea adha ya kufuata matibabu umbali mrefu.
Zahanati inayotajwa kugharimu Sh. Milioni 90 ambayo sasa iko kwenye hatua ya msingi, inatarajiwa kukamilika mwaka huu na kuanza kutoa huduma kwa wananchi hao.
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, amewapongeza wananchi wa kijiji hicho leo baada ya kufanya ziara ya kutembelea na kukagua ujenzi huo wa Zahanati, akiwa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga, Hoja Mahiba na baadhi ya maofisa wa Polisi, ambapo Serikali iliahidi kuwaunga mkono ili kukamilisha zahanati hiyo.
Amesema ni jambo la pongezi kwa wananchi kujitoa wenyewe kuchangia shughuli za maendeleo, ili kutatua baadhi ya changamoto ambazo zinawakabili kuliko kuitegemea Serikali kwa kila kitu, ambapo Zahanati hiyo itakapo kamilika, mbali na kuwaondolea adha ya kufuata matibabu umbari mrefu, pia watapunguza vifo vitokavyo na uzazi.
“Nawapongeza sana wananchi wa Nyaligongo kwa ujenzi huu wa Zahanati ambayo itawasaidia kupata huduma za matibabu karibu na kuimarisha afya zenu, ikiwamo kupunguza vifo vya uzaziwa wakati wa kujifungua, na mama akiwa na afya nzuri na nyumbani pana kuwa safi,”anasema Mboneko.
Naye Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga, Hoja Mahiba, amewapongeza wananchi hao kwa kuanzisha ujenzi huo wa Zahanati, na kubainisha kuwa Sera ya afya inasema kuwepo na Zahanati kwa kila kijiji, ambapo miradi hiyo inafaa kuanza kuibuliwa na wananchi wenyewe na kisha Serikali inawaunga mkono kuikamilisha.
Aidha Mwenyekiti wa Kijiji cha Nyaligongo, Masumbuko Lushona, amesema walifanya mkutano wa hadhara na wananchi na kuhamasishana kuchanga pesa ili kuanza ujenzi wa Zahanati kwenye kijiji hicho, kutokana na kuteseka kufuata huduma ya afya umbari mrefu.
Kwa upande wake Mtendaji wa Kata ya Mwakitolyo Samson Lutonja, amesema ujenzi huo wa Zahanati upo kwenye hatua ya Msingi, ambapo unatarajiwa kukamilika mwaka huu kwa gharama ya Sh. Milioni 90.
Nao baadhi ya akina mama Mary Benjamini, wamesema ujenzi wa Zahanati hiyo utakuwa msaada kwao, na kueleze kuwa huduma ya matibabu inapokuwa mbali wanaoteseka hua ni wanawake pamoja na watoto.
TAZAMA PICHA HAPA CHINI
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, akizungumza na wananchi wa kijiji cha Nyaligongo Kata ya Mwakitolyo wilayani Shinyanga, na kuwapongeza kuanzisha ujenzi wa Zahanati.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, akizungumza na wananchi wa kijiji cha Nyaligongo Kata ya Mwakitolyo wilayani Shinyanga, na kuwapongeza kuanzisha ujenzi wa Zahanati.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga, Hoja Mahiba akizungumza kwenye ujenzi wa Zahanati ya kijiji cha Nyaligongo ambayo imeanzishwa kujengwa na wanachi wenyewe.
Diwani wa Kata ya Mwakitolyo, Masalu Nyese, akizungumzia ujenzi huo wa Zahanati namna walivyo hamasishana na Wananchi kuanza kuijenga.
Afisa Mtendaji wa Kata ya Mwakitolyo, Samson Lutonja, akizungumzia ujenzi huo wa Zahanati ya kijiji cha Nyaligongo.
Mary Benjamini mkazi wa kijiji cha Nyaligongo, akielezea umuhimu wa Zahanati hiyo kwenye kijiji hicho.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko akikagua ujenzi wa Zahanati ya kijiji cha Nyaligongo.
Muonekano wa Msingi ujenzi wa Zahanati kijiji cha Nyaligongo.