Azza Hilal akiwa anaomba kura za maoni kuwania ubunge jimbo la Solwa mkoa wa Shinyanga mwaka 2020
Rais Samia Suluhu Hassan leo Mei 29, 2021 amefanya uteuzi wa baadhi ya makatibu tawala wa mikoa, kuwahamisha baadhi na wengine kuwabakisha kwenye vituo vyao vya kazi. Miongoni mwa walioteuliwa ni aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalum (CCM) mkoa wa Shinyanga, Azza H. Hilal ambaye ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa mkoa wa Simiyu.
Azza ameteuliwa baada ya kushindwa kwenye kura za maoni ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuwania ubunge wa Jimbo la Solwa mkoani Shinyanga katika mchakato wa uchaguzi mkuu mwaka jana.