BALOZI BATILDA BURIANI NDIYE KATIBU TAWALA MPYA MKOA WA SHINYANGA


Balozi Dk. Batilda Buriani

Na Shinyanga Press Club Blog
Leo Mei 29, 2021 Balozi Dk. Batilda Buriani ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga akichukua nafasi ya Albert Msovela ambaye amehamishiwa mkoa wa Mara.

Balozi Dk. Batilda kabla ya uteuzi huo alikuwa Balozi wa Tanzania nchini Japan mwaka 2015 - 2016 na Kenya mwaka 2012 - 2015.

Pia amekuwa Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuanzia mwaka 2000 hadi 2010 kabla ya kuangushwa kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 na Godbless Lema wa Chadema katika jimbo la Arusha Mjini.
 
Katika kipindi chake cha ubunge, aliwahi kuwa Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto ambayo kwa sasa ni Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto.

Vilevile, akawa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) wakati wa serikali ya awamu ya nne.

Balozi Dk. Batilda Buriani




Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464