Aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalum CCM Mkoa wa Shinyanga, Azza Hilal Hamad
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ametengua uteuzi wa Azza Hilal Hamad kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu na nafasi yake kuchukuliwa na Prisca Joseph Kayombo ambaye alikuwa Afisa Mkuu wa Utawala na Utumishi katika Wizara ya Fedha na Mipango.
Bi. Azza aliteuliwa jana Mei 29, 2021 kushika wadhifa wa Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, ambapo sasa kwa mujibu wa Taarifa ya Ikulu iliyotolewa usiku huu, Azza atapangiwa majukumu mengine.