Tanzania leo imeungana na Mataifa mengine Duniani kuadhimisha siku ya Mama ambapo Shirika lisilo la Kiserikali la Wekeza kwa Watoto na Jamii (ICS) limeadhimisha kwa namna tofauti kwa kutoa elimu kwa jamii juu ya kuthamini mchango wa Mama.
Elimu hiyo imetolewa katika Kijiji na kata ya Bukene Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga ambapo Mkurugenzi wa Shirika la(ICS) Bw. Kudely Sokoine ameitaka jamii kujenga tabia ya kutambua mchango wa mama kwenye malezi na makuzi ya familia yoyote.
Kudely amesema ili jamii ijengwe katika uelewa mkubwa wa kuona thamani ya Mama lazima ianzie ngazi ya familia, watoto wakiwa wangali wadogo wajengewe uwezo wa kutambua thamani ya mama ambaye ana jukumu kubwa katika familia.
Akizungumza na Shinyanga blog mmoja wa watoto Agape Evaliste amesema kuwa kuna umuhimu wa kumtunza mama pale anapokuwa amefanya kazi nzuri na inayoonekana kwa jamii hupaswa kupongezwa tabia ambayo hupaswa kujegwa wakiwa wadogo.
kwa upande wao baadhi ya fulsa ya kueleza nafasi ya teknolojia ya mawasiliano katika kuimarisha mawasiliano, Elias Moses amesema kuwa ujio wa teknolojia ya habari na mawasiliano katika maeneo yao hususani simu na Luninga imechangia kwa kiwango kikubwa kufikia maendeleo na kukuza mahusiano katika jamii,sambamba na kufikisha ujumbe kwa haraka.
Moses ameongeza kwa kusema kuwa maeneo ya vijijini yalisahaulika kwa muda hivyo ujio wa simu na luninga umewafanya na wao kuwa sehemu ya jamii za kitanzania na kuendana na dunia ya mabadiliko ya sayansi na teknolojia sanjali na kukuza ucumi wao kwa kuwa simu imekuwa ikitumika katika kuwasiliana na wateja wao.
Kauli ya Moses inaungwa mkono na Paulo Mmdege ambaye amesema kuwa mawasiliano ya simu kwake yamekuwa msaada mkubwa wa kuwasiliana na ndugu zake walioko mbali hali inayochangia kutatua changamoto za familia kwa wakati.
Kwa upande wake Eva Joseph amesema kuwa ujio wa mawasiliao ya simu kumesababisha migogoro mingi kwa baadhi ya familia kutokana na wengi wa wanaume kutumia muda mwingi kuchati, badala ya kuzungumza na familia zao hali inayoleta utengano kwenye maisha ya kila siku.
Naye Maria Mathayo ameongeza kuwa kutokana na mila na desturi zao, wanaume wengi kwa sasa wanatumia muda wao mwingi kwenye simu kuliko kujishulisha na uzalishaji mali, na kuwaacha wanawake kuwa wazalishaji wakuu ambao hawewezi kuzalisha chakula cha kukidhi jamii au familia nzima.
Akihitimisha mjadala wa elimu juu ya mapokeo ya teknolojia kwa jamii, Mkurugenzi wa Shirika la(ICS) Bw Kudely Sokoine amesema kuwa katika utafiti wao mdogo wamebaini kuwa ujio wa teknolojia maeneo ya vijijini umechangia kwa kiwango kikubwa mmonyonyoko wa maadili kwenye jamii.
Aidha Kudely amesema licha ya maadili kummonyonyoka pia watoto wengi kwa sasa hutumia muda huo kuangalia simu na tv badaa ya kusoma ili kuandaa maisha yao ya baadaye.
Siku ya Mama uadhimishwa kila ifikapo May 9, ya kila mwaka ikiwa ni kukumbuka na kuthamini mchango wa mama kwenye jamii kwa kuzinagatia kuwa mama ana uwezo wa kufanya kazi zaidi ya 3 kwa wakati mmoja ambapo Shirika la (ICS) limeadhimisha kwa kutoa elimu katika Kijiji na Kata ya Bukene Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga.