MAONESHO YA BIDHAA ZA WAJASIRIAMALI NA WAWEKEZAJI KAHAMA KUWAKUTANISHA WAFANYABIASHARA 250 WAKISAKA MASOKO YA UHAKIKA

Mkuu wa wilaya ya Kahama Mhe. Anamringi Macha akielezea kuhusu Maonesho ya Wajasiriamali na Wawekezaji yatakayofanyika kuanzia Jumatatu Mei 24,2021 hadi Mei 30,2021 katika Kituo cha Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi kilichopo Nyihogo Mjini Kahama.

Na Kadama Malunde - Kahama
Zaidi ya Wajasiriamali na Wawekezaji 250 wanatarajiwa kushiriki katika Maonesho ya bidhaa za Wajasiriamali na Wawekezaji yatakayofanyika kuanzia Kesho Jumatatu Mei 24,2021 hadi Mei 30,2021 katika viwanja vya Kituo cha Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi Nyihogo Mjini Kahama.

Maonesho hayo ya Wajasiriamali na Wawekezaji yaliyoandaliwa na Kituo cha Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi Kahama yana lengo la kuonesha bidhaa za wajasiriamali,kuwapa elimu namna ya kufungasha bidhaa,urasimishaji biashara,kufungua fursa za masoko, kukipa nguvu na kukitangaza Kituo cha Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi Kahama na fursa zingine kadha wa kadha.

Akizungumza na Waandishi wa Habari Mei 22,2021, Mkuu wa wilaya ya Kahama Mhe. Anamringi Macha amewasihi Wajasiriamali, Wafanyabiashara na Wawekezaji kutumia maonesho hayo kutangaza bidhaa zao pamoja kuongeza ujuzi utakaowafanya kufanya vizuri katika biashara zao.

“Maonesho haya ya fursa nyingi, wajariamali wataonesha bidhaa wanazozalisha na tutaleta wataalamu watakaotoa elimu kwa wajasiriamali kupitia semina na makongamano mbalimbali yatakayoendeshwa. Serikali inataka kuondoa kitu kinaitwa Wanyonge, tunataka tuondoe kada ya unyonge tuwe na watanzania wenye hali nzuri kiuchumi”,amesema Macha.

Mkuu huyo wa wilaya pia amewashauri wajasiriamali kuwaza sehemu za kupata masoko kabla ya kuzalisha bidhaa kwa kuangalia msimu hivyo kuwataka watumie Kituo cha Uwezeshaji wananchi kiuchumi Kahama kwa ajili ya kupata usaidizi wa namna ya kufanya biashara zao kwa tija zaidi.

“Kituo cha Uwezeshaji wananchi kiuchumi kimeanzishwa kwa lengo la kuwarahishia wananchi kupata huduma,wasajiliwe, lengo ni kuendelea kuona bidhaa za wajasiriamali wale ambao hawajafanikiwa wanainuka kiuchumi. Tunataka bidhaa ziende kwenye maduka,tutambue mahali wanapotengenezea bidhaa na tuwafahamu wazalishaji”,amesema Macha.

“Niwapongeze sana GS1 Tanzania na TCCIA pamoja na taasisi zingine zilizoshiriki kuandaa maonesho haya. Tunataka kuweka mabanda ya kudumu hapa kwa ajili ya kuonesha bidhaa zetu kila siku na kutafuta masoko kwa wajasiriamali wetu. Hapa pawe mahali pa maonesho, watu wa Benki wakiona watakuwa tayari kutoa mikopo kwa wajasiriamali”,ameongeza Macha.

Kwa upande wake Mratibu wa Maonesho ya Wajasiriamali na Wawekezaji Kahama, Shaban Mikongoti ambaye ni Afisa Masoko wa Taasisi ya GS1 Tanzania, amesema Mwaka huu 2021 GS1 Tanzania inasherehekea miaka 10 ya kuanzishwa kwake hivyo katika kufanikisha maadhimisho hayo, GS1 Tanzania imeamua kushirikiana na taasisi mbalimbali zilizopo katika Kituo cha Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi wilaya ya Kahama.

“Kutokana na umuhimu wa Kituo cha Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi tumeona ni umuhimu wa kituo hiki hususani kwa wananchi wa Kahama na Kanda ya Ziwa kwa ujumla kuna haja ya kufanya Maadhimisho ya miaka 10 ya Taasisi ya Kimataifa isiyotengeneza Faida ya GS1 Tanzania kwa kufanya maonesho ya Wajasiriamali na Wawekezaji kwa lengo la kuwajengea uwezo Wafanyabiashara na wajasiriamali wadogo na kuwapatia masoko ya uhakika”,ameeleza Mikongoti.

“Wafanyabishara watapata fursa ya masoko na kujifunza,lakini pia tumealika wafanyabiashara wakubwa na wawekezaji watakaotoa ujuzi ili wafanyabiashara wa Kahama waweze kuingia kwenye ushindani.Tutafanya maonesho lakini pia tutakuwa na semina mbalimbali na mashindano mbalimbali ya vipaji katika eneo la maonesho”,amesema.

Amefafanua kuwa Maonesho hayo yanafanyika katika mikoa 10 nchini Tanzania na kwa upande wa Shinyanga yanafanyika Kahama kwa kushirikiana na taasisi wezeshi zilizopo katika kituo cha uwezeshaji wananchi kiuchumi Kahama.

“Tunahitaji kukitangaza kituo cha Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi Kahama ili wananchi wazifahamu fursa zilizopo katika kituo hiki tuliona umuhimu wa kuwepo kwa maonesho haya ili wananchi wa Kahama wapate fursa ya kupata mafunzo mbalimbali ikiwemo kurasimisha makampuni na majina ya biashara na kuongeza thamani ya bidhaa zao”,amesema.

“Kituo cha Uwezeshaji wananchi Kiuchumi hiki kina fursa kubwa na kina taasisi zote wezeshi za kuhamasisha wafanyabiashara kushindana na kuwajengea uwezo kwa maana hiyo Kahama ina fursa za kipekee imepata kituo hiki ili wakitumie kwa ufanisi mkubwa kwa sababu ndiyo kituo chenye taasisi zote nchini”,ameongeza Mikongoti.

Amesema katika maonesho hayo pia kutakuwa na kongamano la kujadili fursa mbalimbali za uwekezaji na fursa za kufanya biashara ambapo wamewaalika wawekezaji na wafanyabiashara wakubwa kwa ajili ya kuwasaidia wafanyabiashara wadogo.

Naye Mwenyekiti wa Kamati ya Maonesho ya Wajasiriamali na Wawekezaji Kahama, Simon Cheyo ameishukuru Kampuni ya Barrick, TRA, NMB, Pass Trust na taasisi zingine kwa kudhamini maonesho hayo na kwamba maandalizi yote yamekamilika.

“Eneo la maonesho ni salama, kwa wale watakaoshiriki eneo halina gharama, karibuni mlete bidhaa zenu, sehemu za kulala zipo karibu na eneo la maonesho.Tunatamani tusiishie kwenye kuonesha bidhaa tu, bali tujifunze zaidi, tumeita watu wa viwanda kuja kutoa elimu. Tunawashukuru wadau wote, wale wanaokuja tunawakaribisha sana, tupo muda wote”, amesema Cheyo.

Cheyo ambaye pia Afisa Mtendaji wa Chemba ya Wafanyabiashara, Wakulima na Watu wenye Viwanda (TCCIA) wilaya ya Kahama, amemshukuru Mkuu wa wilaya ya Kahama Mhe. Anamringi Macha kwa kuendelea kuwa karibu na kituo cha Uwezeshaji wananchi Kiuchumi Kahama kwani amekuwa mshauri akiwa amebeba maono makubwa na amekuwa akitembelea kituo hicho mara kwa mara.

ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Mkuu wa wilaya ya Kahama Mhe. Anamringi Macha akielezea kuhusu Maonesho ya Wajasiriamali na Wawekezaji yatakayofanyika kuanzia Jumatatu Mei 24,2021 hadi Mei 30,2021 katika Kituo cha Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi kilichopo Nyihogo Mjini Kahama. Kulia ni Kaimu Mwenyekiti wa Kituo cha Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi Kahama, Oscar Damas, Kushoto ni Mwenyekiti wa Kamati ya Maonesho ya Wajasiriamali na Wawekezaji Kahama, Simon Cheyo. 
Mkuu wa wilaya ya Kahama Mhe. Anamringi Macha akielezea kuhusu Maonesho ya Wajasiriamali na Wawekezaji yatakayofanyika kuanzia Jumatatu Mei 24,2021 hadi Mei 30,2021 katika Kituo cha Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi kilichopo Nyihogo Mjini Kahama.
Mratibu wa Maonesho ya Wajasiriamali na Wawekezaji Kahama, Shaban Mikongoti ambaye ni Afisa Masoko wa Taasisi ya GS1 Tanzania akielezea kuhusu Maonesho ya Wajasiriamali na Wawekezaji yatakayofanyika kuanzia Jumatatu Mei 24,2021 hadi Mei 30,2021 katika Kituo cha Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi kilichopo Nyihogo Mjini Kahama.

Mwenyekiti wa Kamati ya Maonesho ya Wajasiriamali na Wawekezaji Kahama, Simon Cheyo akielezea kuhusu Maonesho ya Wajasiriamali na Wawekezaji yatakayofanyika kuanzia Jumatatu Mei 24,2021 hadi Mei 30,2021 katika Kituo cha Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi kilichopo Nyihogo Mjini Kahama.

Kaimu Mkuu wa Kituo cha Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi Kahama, Oscar Damas akielezea kuhusu Maonesho ya Wajasiriamali na Wawekezaji yatakayofanyika kuanzia Jumatatu Mei 24,2021 hadi Mei 30,2021 katika Kituo cha Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi kilichopo Nyihogo Mjini Kahama. Kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Kahama Mhe. Anamringi Macha, kulia ni Mratibu wa Chuo Huria Kahama, Lucas Mafuru
Wadau wakisikiliza taarifa kuhusu Maonesho ya Wajasiriamali na Wawekezaji yatakayofanyika kuanzia Jumatatu Mei 24,2021 hadi Mei 30,2021 katika Kituo cha Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi kilichopo Nyihogo Mjini Kahama.

Mkuu wa wilaya ya Kahama Mhe. Anamringi Macha akipiga picha ya kumbukumbu na Wajumbe wa Kamati ya Maonesho ya Wajasiriamali na Wawekezaji yatakayofanyika kuanzia Jumatatu Mei 24,2021 hadi Mei 30,2021 katika Kituo cha Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi kilichopo Nyihogo Mjini Kahama.
Mkuu wa wilaya ya Kahama Mhe. Anamringi Macha akipiga picha ya kumbukumbu na sehemu ya wadau na wajasirimali watakaoshiriki kwenye Maonesho ya Wajasiriamali na Wawekezaji yatakayofanyika kuanzia Jumatatu Mei 24,2021 hadi Mei 30,2021 katika Kituo cha Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi kilichopo Nyihogo Mjini Kahama.
Mkuu wa wilaya ya Kahama Mhe. Anamringi Macha akipiga picha ya kumbukumbu na baadhi ya viongozi wa taasisi zitakazoshiriki Maonesho ya Wajasiriamali na Wawekezaji yatakayofanyika kuanzia Jumatatu Mei 24,2021 hadi Mei 30,2021 katika Kituo cha Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi kilichopo Nyihogo Mjini Kahama.
Mkuu wa wilaya ya Kahama Mhe. Anamringi Macha (katikati) akikagua eneo la Maonesho ya Wajasiriamali na Wawekezaji yatakayofanyika kuanzia Jumatatu Mei 24,2021 hadi Mei 30,2021 katika Kituo cha Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi kilichopo Nyihogo Mjini Kahama.
Mkuu wa wilaya ya Kahama Mhe. Anamringi Macha akikagua moja ya majukwaa yatakayokuwepo kwenye Maonesho ya Wajasiriamali na Wawekezaji yatakayofanyika kuanzia Jumatatu Mei 24,2021 hadi Mei 30,2021 katika Kituo cha Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi kilichopo Nyihogo Mjini Kahama.

Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464