SHY WOMEN'S DAY OUT YA WOMEN FOR CHANGE YAFANA, AUNT SADAKA, PASTOR MGOGO WATOA UJUMBE

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga Hoja Mahiba, akitoa vyeti kwa wadau ambao wamefadhili Kongamano hilo la wanawake 'Shy Women's Day Out' lililoandaliwa na Women For Change.

Na Marco Maduhu, Shinyanga
Kongamano la Chama Cha Wanawake mkoani Shinyanga, Women For Change 'Shy Women's Day Out' limefanyika mjini Shinyanga kwa kukutanisha wanawake, kubadilishana mawazo pamoja na kupewa masomo mbalimbali ya kuwajenga.

Kongamano hilo limefanyika Mei 30,2021 katika ukumbi wa mikutano wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa Shinyanga, ambapo mgeni rasmi alikuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga, Hoja Mahiba.

Aidha kwenye Kongamano hilo, watoa mada za kuwajenga wanawake, alikuwa mama Edina Shoo, Khadija Liganga, Dkt. Mfaume Salum, Sadaka Gandi (Anti Sadaka) pamoja na Pastor Daniel Mgogo.


Wakizungumza kwa nyakati tofauti, watoa mada hao wamewataka wanawake kujiamini, wajitambue,kupendana, kushikamana, pamoja na kujituma kufanya kazi ili wasiwe tegemezi kutoka kwa waume zao.

Akitoa mada kwenye Kongamano hilo Anti Sadaka, amewataka wanawake wasiwe watumwa wa fikra, na wasishindane na mtu, bali washindane na nafsi zao ndipo watapata kufanikiwa.

Naye mtoa mada Khadija Liganga ,amesema nguvu ya mwanamke ipo kwa mwanamke mwenzake ,hivyo ni vyema washikamane na kushirikiana katika nyanja mbalimbali katika mapambano ya kimaisha.

Mtoa mada mwingine Edna Shoo, amewataka wanawake pale wanapokumbana na matatizo au changamoto mbalimbali, wazipokee pamoja na kuzitafutia ufumbuzi na wasiwe wepesi wa kukata tamaa.

Mchungaji Daniel Mgogo 'Pastor Mgogo' akitoa mada kwenye Kongamano hilo, amewapongeza wanawake kwa kuanza kupendana, kuinuana, kujishughulisha, pamoja na kushikamana, tofauti na miaka ya nyuma ambapo walikuwa na hali mbaya.

"Nawapongeza wanawake kwa kuanza kubadilika na muendelee kupendana na msirudi nyuma, mkichukiana ni furaha kwetu sisi wanaume, kwani mtakwama mambo yenu na tutaendelea kuwatalawa," amesema Mgogo.

Pia Mchungaji Mgogo, amewataka wanawake ambao wamefanikiwa kimaisha wasiwadharau waume zao, pamoja na kuwanyanyasa, bali wawatunze na kuwahudumia kwa kila kitu ikiwamo kuwanunulia mavazi.

Aidha Dkt. Mfaume Salum ambaye ni Daktari bingwa wa magonjwa ya akina mama katika Hospitali ya Rufaa ya mkoa Shinyanga, amewataka akina mama hao, licha ya kujituma katika shughuli za kiuchumi, wasisahau pia kupima afya zao hasa Saratani ya mlango wa Shingo ya kizazi, ambapo wakiiwahi inatibika.

Kwa upande wake mgeni rasmi Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga Hoja Mahiba, amewataka wapinge masuala ya ukatili wa kijinsia ndani ya jamii, pamoja na kuzingatia malezi bora kwa watoto wao.

Katika hatua nyingine Mahiba amewataka wanawake mkoani Shinyanga, wachangamkie mikopo ya Halmashauri asilimia 4 ambayo hutolewa kwa wanawake na haina riba, ili wapate mitaji na kufanya shughuli za kuwainua kiuchumi.

Mwenyekiti wa chama cha wanawake mkoani Shinyanga Women's For Change Getrude Munuo, akisoma risala amesema wapo wanachana 20, na walikianzisha mwaka 2013 na kusajiliwa rasmi mwaka 2014.

Amesema kazi kubwa ambayo wanazifanya ni kusaidiana, na kusaidia pia watu wenye uhitaji zikiwamo na shughuli zingine za kijamii, ambapo mwaka huu wametoa msaada wa madawati katika Shule ya Sekondari Salawe, na kukarabati vyoo kambi ya wazee Usanda wilayani Shinyanga.

Wadau waliofadhili Kongamano hilo Benki ya NMB, NBC, CRDB, Tpb bank, Jambo, Shuwasa, Omyfashion, Shybest, Lulekia, Gvenwear, Fresho, Vai Saloon, Nuru Fashion, Wine Keki, Bomba Security na Tahosa Stationary.

Wadau wengine ni Shule za Little Treasures, Chuo cha afya Kolandoto, Sene Open Business, Virgmark na Karena Hotel, Love Decoration,Vivak Investment, VRK Trader,Kanvolpics, Diamond Autolink, VIHAS, fk , Manka Electronics, Vihas, na Vanson Microfinance.

TAZAMA MATUKIO KATIKA PICHA HAPA CHINI
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga Hoja Mahiba, akizungumza kwenye Kongamano la wanawake mkoani Shinyanga, Women's For Change. Picha na Marco Maduhu
Daktari Bingwa wa Magonjwa ya akina mama kutoka Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Shinyanga Dkt. Mfaume Salum, akitoa mada kwenye Kongamano hilo la wanawake.
Pastor Daniel Mgogo akitoa mada kwenye Kongamano hilo la wanawake.
Anti Sadaka, akitoa mada kwenye Kongamano hilo la wanawake.
Mama Shoo akitoa Mada kwenye Kongamano hilo la wanawake.
Khadija Liganga akitoa mada kwenye Kongamano hilo la wanawake.
Mwenyekiti wa Chama cha Women's For Change Getrude Munuo, akizungumza kwenye Kongamano hilo la wanawake.
Mwenyekiti wa Kongamano hilo Faustina Kifambe, akizungumza kwenye Kongamano hilo la wanawake Shy Women's Day Out.
Wanachama wa Women's For Change wakiwa kwenye Kongamano la Shy Women's Day Out.
Wanawake wakiwa kwenye Kongamano la Shy Women's day Out.
Kongamano la wanawake likiendelea.
Kongamano la wanawake likiendelea.
Kongamano la wanawake likiendelea.
Kongamano la wanawake likiendelea.
Kongamano la wanawake likiendelea.
Kongamano la wanawake likiendelea.
Kongamano la wanawake likiendelea.
Kongamano la wanawake likiendelea.
Kongamano la wanawake likiendelea.
Kongamano la wanawake likiendelea.
Kongamano la wanawake likiendelea.
Kongamano la wanawake likiendelea.
Kongamano la wanawake likiendelea.
Kongamano la wanawake likiendelea.
Kongamano la wanawake likiendelea.
Kongamano la wanawake likiendelea.
Awali Mgeni Rasmi Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga Hoja Mahiba akiwa na Mwenyekiti wa Chama cha Women's For Change,Getrude wakikata Keki kufungua Kongamano la Wanawake, Shy Women's day Out.
Zoezi la utoaji vyeti wa wafadhili wa Kongamano hilo likiendelea.
Zoezi la utoaji vyeti wa wafadhili wa Kongamano hilo likiendelea.
Zoezi la utoaji vyeti wa wafadhili wa Kongamano hilo likiendelea.
Zoezi la utoaji vyeti wa wafadhili wa Kongamano hilo likiendelea.
Zoezi la utoaji vyeti wa wafadhili wa Kongamano hilo likiendelea.
Zoezi la utoaji vyeti wa wafadhili wa Kongamano hilo likiendelea.
Zoezi la utoaji vyeti wa wafadhili wa Kongamano hilo likiendelea.
Zoezi la utoaji vyeti wa wafadhili wa Kongamano hilo likiendelea.
Zoezi la utoaji vyeti wa wafadhili wa Kongamano hilo likiendelea.
Zoezi la utoaji vyeti wa wafadhili wa Kongamano hilo likiendelea.
Zoezi la utoaji vyeti wa wafadhili wa Kongamano hilo likiendelea.
Zoezi la utoaji vyeti wa wafadhili wa Kongamano hilo likiendelea.
Zoezi la utoaji vyeti wa wafadhili wa Kongamano hilo likiendelea.
Zoezi la utoaji vyeti wa wafadhili wa Kongamano hilo likiendelea.
Zoezi la utoaji vyeti wa wafadhili wa Kongamano hilo likiendelea.
Burudani zikitolewa kwenye Kongamano hilo la wanawake huku wanawake wakipiga Selfie na Pastor Mgogo
Burudani ikiendelea
Wanachama wa Women For Change wakiwa katika picha ya Pamoja na watoa mada kwenye Kongamano la Wanawake Mkoani Shinyanga( Shy Women's Day Out), pamoja na mgeni Rasmi Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga Hoja Mahiba.
Wafadhili wa Kongamano hilo la Wanawake wakipiga picha ya Pamoja na Mgeni Rasmi pamoja na watoa mada.
Picha za pamoja zikipigwa kwenye Zuria Jekundu na watoa mada kabala ya kuanza Kongamano la wanawake "Shy Women's day Out"
Wanachama wa Womens' For Change, wakipiga picha ya pamoja na mgeni rasmi Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga Hoja Mahiba, wa pili kutoka kulia.

Picha zote na Marco Maduhu


Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464