Watumishi wa Taasisi ya Utafiti wa Kilimo (TARI) wakionyesha baadhi ya mazao mbalimbali wakati wa maonyesho ya Sayansi, Teknolojia na ubunifu kwenye uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma
Na Mwandishi wetu, Dodoma
TAASISI ya Utafiti wa Kilimo nchini (TARI) imebainisha kuwa sababu za kilimo cha zao la Pamba kutokubali katika mkoa wa Dodoma baada ya kuanzishwa miaka miwili iliyopita katika wilaya za Chemba, Bahi na Chamwino ni kutokana na changamoto za hali ya hewa ambazo haziendani na kilimo cha zao hilo.
Mwishoni mwa mwaka 2018 Bodi ya Pamba (TCB) chini ya wataalamu wake walizunguka katika wilaya hizo kuwahamasisha wananchi kulima Pamba.
Hata hivyo matokeo hayakuwa mazuri licha ya hamasa kubwa waliyokuwa nayo wananchi ambapo TARI inaeleza kuwa changamoto ya hali ya hewa ikiwamo ikolojia ya mkoa wa Dodoma kutoendana na kilimo cha zao hilo.
Mkurugenzi Mkuu wa TARI, Dk. Geofrey Mkamilo amebainisha hayo katika viwanja wa Jamhuri yanapoendelea maonesho ya kitaifa ya Sayansi, Teknolojia na Ubunifu ambapo Taasisi inashiriki kuonesha namna Teknolojia inavyotumika kuchochea mapinduzi ya kilimo nchini.
Kwa mwaka wa pili sasa TARI imekuwa na idara maalum usambazaji teknolojia ambapo inajivunia kutumia idara hiyo kusambaza teknolojia kwa wakulima nchini kupitia kwa maafisa gani.
Maonesho hayo ya kitaifa ya sayansi na teknolojia na ubunifu nchini yameingia siku ya pili leo, ambapo Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI) inaendelea kuonyesha bidhaa zinazotengenezwa katika vituo vyake vyote nchini huku watafiti kutoka vituo 17 nchini wakiendelea kutoa elimu kwa wananchi wa dodoma
Maofisa wa TARI wakionyesha bidhaa zinazotengenezwa katika vituo vyake vyote nchini
Maonyesho ya bidhaa yakiendelea
Maofisa hao wakionyesha bidhaa zinazotengenezwa katika vituo vyake vyote nchini na kutoa elimu kwa wananchi wa Dodoma
Mbegu za mazao mbalimbali ya kilimo zinazozalishwa na TARI zikionyeshwa kwenye maonyesho ya sayansi, teknolojia na ubunifu katika uwanja wa Jamhuri, Dodoma
Mbegu na bidhaa mbalimbali za mazao zinazozalishwa na TARI zikionyeshwa kwenye maonesho ya sayansi, teknolojia na ubunifu leo katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma
Watendaji wa TARI wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa maonesho hayo
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464