ACP Debora Magiligimba
Na Shinyanga Press Club Blog
KAMANDA wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga, ACP Debora Magiligimba amehamishiwa mkoa wa kipolisi Ilala Kanda Maalum ya Dar es Salaam akichukua nafasi ya ACP Janeth Magomi anayeenda kuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe.
Nafasi ya ACP Magiligimba itachukuliwa na Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP), George Kyando aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe.
Mabadiliko hayo yametangazwa leo Juni 4, 2021 jijini Dodoma na Msemaji wa Jeshi la Polisi Nchini, SACP David Misime katika mkutano wake na waandishi wa habari alipokuwa akitoa taarifa kwa vyombo vya habari juu ya mwenendo wa kesi 10 za unyanyasaji katika mikoa sita nchini.
ACP Magiligimba atakumbukwa kwa kazi kubwa aliyoifanya katika mkoa wa Shinyanga ikiwemo vita dhidi ya ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watoto, mapambano ambayo yalileta matunda mbalimbali kwa jamii na kwake binafsi ikiwemo kutunukiwa zawadi mbalimbali.
TAZAMA HAPA CHINI TAARIFA HIYO