Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) Sylvester Mwakitalu akipokea Maelezo kutoka kwa Mkuu wa Gereza la Mahabusu Segerea Mrakibu Mwandamizi wa Magereza(SSP)Daniel Mwakyoma wakati alipotembelea Gereza hilo Juni 13,2021.
Mkurugenzi wa Mashtaka Nchini (DPP)
Sylvester Mwakitalu amehitimisha ziara yake ya kutembelea na kukagua hali ya Magereza ya Mkoa wa Dar es Salaam baada ya kutembelea na kuzungumza
na Mahabusu pamoja na wafungwa walioko katika magereza yote matatu ya mkoa huo.
Akizungumza mara baada ya
kujionea hali ilivyo katika Magereza hayo, baada ya kuhitimisha ziara kwa kutembelea
Gereza la Mahabusu Segerea DPP Mwakitalu
amesema Changamoto alizoziona ndani ya
magereza hayo zitamsadia katika kufanya maamuzi na kuboreha utendaji kazi wa
Ofisi ya Taifa ya Mashtaka.
DPP Mwakitalu alisema
changamoto zilizowasilishwa na baadhi ya mahabusu walioko gereza la Segerea
ambazo hazipo ndani ya uwezo wa Ofisi ya
Mashtaka atakahikikisha anazifikisha kwa wahusika ili ziweze kutafutiwa
ufumbuzi ambapo amesema maeneo yanayohitaji suluhisho la pamoja atahakikisha
anakaa na wadau ili kutafuta suluhisho la pamoja.
“Kwa changamoto ambazo ziko
chini ya ofisi yangu, nitazifanyia kazi kwa
haraka kadri iwezekanavyo ili haki
iweze kutendeka,haya mengine
ambayo yako nje ya Ofisi yangu nitawashirikisha wadau wakiwemo mahakama,
wapelelezi na wachunguzi ili tuwe na suluhu ya pamoja”Alisema DPP Mwakitalu
Aidha, DPP Mwakitalu akizugumzia
chagamoto ya kuchelewa kwa upelelezi wa mashauri mbalimbali alisema kuwa wapelelezi
wanaoshugulikia kesi ni wadau wake wa karibu
kwani bila uwepo wao yeye hawezi kufanya kazi hivyo ameahidi kukaa kwa
pamoja ili kesi zilizoko mahakamani ambazo
upelelezi wake haujakamalika uweze kufika mwisho.
Alisema Ofisi ya Taifa ya Mashtaka katika kutekeleza
majukumu yake itaendelea kufanya kazi zake kwa kutenda haki.
Mwakitalu alisema kuwa kwa sasa Ofisi yake kwa pamoja na watendaji
wataanza kazi ya kupitia upya majalada ya kesi ili kubaini kama yana ushahidi
wa kutosha kesi ziendelee na kama ushahidi wake ni hafifu atayafanyia maamuzi.
“Naomba niwaeleze
changamoto hizi na ushauri wenu nimeupokea kwa sasa hatua tulizonazo ni kupitia upya majalada ya kesi
ili kuona lipi linafaa kuendlea a lipi linafaa kufanyiwa maamuzi upya”alisema
DPP Mwakitalu
Katika hatua nyingine DPP alisema kuwa Ofisi yake kwa
sasa itahikikisha inapeleka kesi
mahakamani zenye ushahidi kamili na zile ambazo bado hazijapata Ushaihidi
kamili hazitafikishwa Mahakamani ili kuondoa changamoto ya Msongamano Magerezani .
Kuhusiana na suala la utoaji wa vibali vya kesi DPP
Mwakitalu alisema kuwa atahakikisha vibali vya Kesi(Concert) ambazo zimekwama kutokana na kukosa kibali
hicho atahakikisha vibali hivyo
vinatolewa ili kesi ziweze kuendelea.
Aidha, DPP Mwakitalu ametembelea magareza ya Keko,Segerea
na Gereza Kuu Ukonga ambapo alisema kuwa huo ni Mwendelezo wa ziara zake za
kutembelea na kukagua hali ya magereza hapa nchini, kusikiliza kero na changamoto za wafungwa na mahabusu ili
Ofisi yake iweze kuzitafutia Suluhu
Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) Sylvester Mwakitalu akiwasili katika gereza la Mahabusu Segerea na kupokelewa na mkuu wa gereza hilo Mrakibu Mwandamizi wa Magereza Daniel Mwakyoma Mapema juni 13,2021.Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) Sylvester Mwakitalu(Kushoto)akisalimiana na Mkuu wa Gereza la Mahabusu wanawake Segerea Mrakibu wa Magereza Iyunge Saganda (wa pili kutoka kushoto) wakati wa ziara ya kutembelea na kusikiliza changamoto za Mahabusu .
Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) Sylvester Mwakitalu akisalimiana na baadhi ya maafisa wa magereza katika gereza la Mahabusu Segerea Mkoani Dar es salaam wakati wa ziara yake.Mkuu wa Gereza la Mahabusu Segerea Mrakibu Mwandamizi wa Magereza(SSP)Daniel Mwakyoma akiwaongoza Viongozi kutoka Ofisi ya Taifa ya Mashtaka wakiongozwa na Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP)Sylvester Mwakitalu kuelekea Gereza la Mahabusu wanaume.