Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi, Khamis Hamza Chilo akilikagua basi la Kampuni ya Classic ambalo lilipata ajali wilayani Shinyanga na kuua watu wanne na kujeruhi wengine 20
Na Shinyanga Press Club Blog
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi ambae pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Khamis Hamza Chilo, usiku wa kuamkia leo ametembelea eneo la ajali iliyohusisha basi la abiria la kampuni ya Classic linalofanya safari zake kati ya Kampala Uganda na Dar es Salaam na kuelezwa chanzo cha ajali hiyo.
Ajali ya basi hilo ambalo lilikuwa limebeba baadhi ya wanafunzi wa Tanzania wanaosoma katika Chuo Kikuu cha Bugema nchini Uganda, ilitokea saa 10:54 Alfajiri ya Juni 2, 2021 katika eneo la Buyubi Kata ya Didia wilaya ya Shinyanga mkoani humo na kuua watu wanne na kujeruhi wengine 20wakiwemo watano ambao viungo vimekatika.
Tayari miili ya watu wanne waliofariki kwenye ajali hiyo imesafirishwa kwenda Zanzibar, huku majeruhi 15 wakitibiwa na kuruhusiwa
Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi