RC SENGATI AZUNGUMZA NA WAZEE WA SHINYANGA, CHANGAMOTO ZA MABARAZA, MATIBABU, MIKOPO, KUTELEKEZWA NA FAMILIA ZAIBULIWA…. AWAAHIDI MAKUBWA

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Dkt. Philemon Sengati akizungumza kwenye kikao chake na Wazee wa Mkoa wa Shinyanga leo Alhamis Juni 17,2021 katik ukumbi wa CCM mkoa wa Shinyanga.

Na Damian Masyenene, SHINYANGA
MKUU wa Mkoa wa Shinyanga, Dk. Philemon Sengati leo Juni 17, 2021 amekutana na kuzungumza na wazee wa mkoa huo katika ukumbi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika kikao kilichohudhuriwa pia na Kaimu Katibu tawala, Balozi Dk. Batilda Buriani, Mwenyekiti wa CCM mkoani humo, Mabala Mlolwa, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, ACP George Kyando, Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Jasinta Mboneko, Mkuu wa Wilaya ya Kishapu, Nyabaganga Talaba,  na wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama na ile ya amani.

Mkutano huo ulikusudia kusikiliza changamoto zinazowakabili wazee na namna ya kuwashirikisha katika ujenzi wa uchumi wa mkoa wa Shinyanga lakini pia kuendeleza maono ya Rais Samia Suluhu Hassan kukutana na makundi mbalimbali kwenye jamii, Mkuu huyo wa mkoa ameahidi kuendelea kukutana na wazee hao, vijana na akina mama.

Akizungumza na wazee kutoka wilaya za Kahama, Shinyanga na Kishapu, Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Dk. Philemon Sengati, ametoa maelekezo mabaraza ya wazee ambayo yamekufa yafufuliwe, huku akiwataka wakurugenzi wote wa halmashauri za mkoa huo kuendelea kuyawezesha mabaraza hayo na kutenga fedha kwa ajili ya kuwezesha afua za wazee na kamwe hatokuwa mvumilivu kuona halmashauri inalega katika kuwezesha wazee.

“Naelekeza pia ofisi ya mkuu wa mkoa kwa wazee wetu na viongozi wa dini wakija waruhusiwe kuingia mara moja na siyo kukalishwa kwenye benchi kusubiri foleni. Wazee tunaomba mawazo yenu chanya tuweze kuujenga uchumi wa mkoa wetu, nami niko tayari kufanya akzi nanyi muda wote,” ameelekeza.

Dk. Sengati pia amemuelekeza Kamanda wa Polisi wa mkoa huo kuhakikisha kuwa hakuna mzee hata mmoja atakayeuawa ndani ya mkoa wa Shinyanga, huku akibainisha kwamba wamepanga kusimamia amani, kujenga umoja, kujenga uchumi wa Shinyanga ili kila mmoja awe na uchumi mzuri na kuchangia pato la taifa na kubadilisha fursa zilizopo Shinyanga kwa ajili ya ustawi wa wananchi na ni lazima wazee washiriki katika kujenga uchumi wa mkoa huo.

“Matukio ya Wazee kuuawa yameshuka, tutaendelea kusimamia hili na nimuelekeze Kamanda wa polisi hatutaki kusikia mzee ameuawa ndani ya mkoa wa Shinyanga. Tunaahidi kushughulikia changamoto zikiwemo za unyanyasaji, kutengwa na kuachiwa kulea familia na kukosa matibabu, kwahiyo naendelea kuwahakikishia kuwa tutaendelea kuwaunganisha wazee waliotelekezwa na familia zao,” ameahidi.

Katika hatua nyingine, RC Sengati amewaahidi wazee hao kuwa wanayo mipango ya kuanzisha chuo kikuu kikubwa kitakachotoa elimu ya juu ili kutoa fursa mbalimbali za ajira, biashara na kukuza uchumi wa mkoa huo.

Awali akisoma risala ya baraza hilo mbele ya Mkuu wa Mkoa, Katibu wa Baraza la Wazee Mkoa wa Shinyanga, Anderson Lyimo ameyataka mabaraza ya wazee katika halmashauri kufanya uhamasishaji kusaidia kuchangia wazee waweze kupatiwa bima za matibabu, huku akiiomba Serikali kuitungia sheria na kanuni zake sera ya taifa ya wazee ya mwaka 2003 ili wazee wapate chombo cha kuwasemea.

Lyimo ameeleza kuwa kwa sasa wazee mkoani humo wanakabiliwa na changamoto za kutelekezwa na familia zao na kushindwa kutunzwa na vijana, vituo vya afya kukosa dawa za kutosha kuwahudumia wazee, baadhi ya mabaraza katika halmashauri kutokuwa hai na viongozi wa mabaraza hayo kutoshirikishwa kwenye maamuzi mengi ya halmashauri, huku halmashauri zikiwa hazijatenga bajeti za kuwategemeza wazee.

Akitoa taarifa ya mkoa huo juu ya wazee, Mwakilishi wa Mganga Mkuu wa Mkoa, Timothy Sosoma ameeleza kuwa mkoa huo unao wazee 66,366 walioandikishwa, kati yao wanaume ni 29,937 na wanawake ni 36,462, ambapo wazee 21,045 sawa na asilimia 31.5 wamepatiwa kadi za bure za matibabu wakiwemo wanawake 12,120 na wanaume 8,925.

Amebainisha kuwa wazee waliopata bima ya afya ya CHF ni 5,571 sawa na asilimia 8.4, ambapo idara ya afya imetenga maeneo ya wazee kwenye vituo vya kutolea huduma yenye ujumbe wa MPISHE MZEE, huku hospitali za wilaya nay a rufaa kukiwa na chumba maalum kwa ajili ya kuwasikiliza wazee.

“Bado tunakabiliwa na changamoto mwitikio mdogo wa utambuaji wazee, kasi ndogo ya utoaji kadi za bure za matibabu na uandikishaji wa kujiunga na bima ya afya ya CHF iliyoboreshwa,” amesema.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Jasinta Mboneko amesema kuwa wataendelea kuwathamini wazee na kuzitambua changamoto zao ili kuzitatua na kueleza kuwa halmashauri ya manispaa ya Shinyanga imetenga jumla ya Sh Milioni 10 kwa ajili ya vitambulisho vya wazee na pia zoezi la kuhakiki kaya mbalimbali kwa ajili ya awamu ya pili ya TASAF kwenye kata zilizosahaulika litaendelea.

Naye Kamanda Mpya wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga, Kamishna Msaidizi wa Polisi George Kyando amewahakikishia wazee hao kuwa jeshi hilo litawalinda na kuwaomba wampee ushirikiano aweze kulinda usalama wa rai ana mali zao.

Wakieleza changamoto mbalimbali zinazowakabili, baadhi ya wazee wamesema kuwa vikao vya mara kwa mara kuzungumza na wazee vishuke hadi ngazi ya chini kwa kuwa huko ndiko kwenye manyanyaso na mahangaiko na kwamba wakifika hospitali dawa hazipo hususan magonjwa yanayowahusu wazee badala yake wanapewa dawa ambazo haziponyi na kaundikiwa wakanunue nje kwenye bei ya juu.

Mzee wa kamati ya ufuatiliaji ngazi ya Manispaa Kahama, Lucy Sodoka ameomba ufanyike utaratibu ngazi ya chini kwa akina mama wazee wanaotelekezewa Watoto ili watambuliwe waweze kusaidiwa kwani wanabebeshwa mizigo mizito, huku pia akiomba kutengenezwa utaratibu maalum wa kuwawezesha wazee miwani ya macho kwani wengi wao wamepoteza nguvu ya kuona.

Naye Shaban Katambi amesema kuwa madirisha ya wazee hayana usimamizi wa kweli kwani wakifika wanakuta hayana huduma na watoa huduma, ambapo ameshauri kuwa kama kuna nia ya dhati ya kuwasaidia wazee basi suala hilo litekelezwe kwa vitendo na siyo kutenga vyumba na madirisha ya wazee ilimradi tu.

Stephano Tano ameshauri kuwa mabaraza ya wazee ni mazuri na yatumike vyema ili kutatua changamoto mbalimbali kwenye jamii, huku Judith Kaswalala mkazi wa Kambarage akieleza kuwa kwenye madirisha ya wazee yaliyoandikwa WAZEE WAPISHWE hawapishwi na hawapewi kipaumbele kwenye huduma za afya kama inayoelezwa.

Akitoa ufafanuzi kwa baadhi ya hoja, Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga, Dk. Ruzila John amesema mwaka huu wamefufua dirisha maalum kwa ajili ya huduma za wazee na yupo daktari mmoja anayesimamia, huku akiwaomba radhi wazee waliokutana na usumbufu hospitali hapo na kuahidi kuwa watakaa kuona namna ya kuliboresha na kuangalia mapungufu ili kuimarisha huduma hiyo.

“Kuna dawa hazipatikani katika bima ya CHF mfano Kisukari na Presha, ni kweli kwa sasa tuna changamoto ya upungufu wa dawa na vifaa tiba lakini serikali kupitia wizara ya afya inaendelea kupambana kuona changamoto hii inaisha,” ameeleza Dk. John.


Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Philemon Sengati akizungumza kwenye kikao chake na Wazee wa Mkoa wa Shinyanga leo Alhamis Juni 17,2021 katik ukumbi wa CCM mkoa wa Shinyanga.Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Philemon Sengati akizungumza kwenye kikao chake na Wazee wa Mkoa wa Shinyanga leo Alhamis Juni 17,2021 katik ukumbi wa CCM mkoa wa Shinyanga
Kaimu Katibu Tawala mkoa wa Shinyanga Balozi Dkt. Batilda Buriani ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Tabora akizungumza kwenye kikao cha Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Philemon Sengati na Wazee wa Mkoa wa Shinyanga leo Alhamis Juni 17,2021 katik ukumbi wa CCM mkoa wa Shinyanga
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akizungumza kwenye kikao cha Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Philemon Sengati na Wazee wa Mkoa wa Shinyanga leo Alhamis Juni 17,2021 katik ukumbi wa CCM mkoa wa Shinyanga
Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Mhe. Nyabaganga Talaba akizungumza kwenye kikao cha Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Philemon Sengati na Wazee wa Mkoa wa Shinyanga leo Alhamis Juni 17,2021 katik ukumbi wa CCM mkoa wa Shinyanga
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga George Kyando akizungumza kwenye kikao cha Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Philemon Sengati na Wazee wa Mkoa wa Shinyanga leo Alhamis Juni 17,2021 katik ukumbi wa CCM mkoa wa Shinyanga
Wazee na wadau wakiwa ukumbini
Katibu wa Baraza la Wazee Mkoa wa Shinyanga ,Anderson Lyimo akisoma risala ya wazee kwenye kikao cha Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Philemon Sengati na Wazee wa Mkoa wa Shinyanga leo Alhamis Juni 17,2021 katik ukumbi wa CCM mkoa wa Shinyanga
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinyanga Mhe. Mabala Mlolwa akizungumza kwenye kikao cha Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Philemon Sengati na Wazee wa Mkoa wa Shinyanga leo Alhamis Juni 17,2021 katik ukumbi wa CCM mkoa wa Shinyanga
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga Mhe. David Nkulila akizungumza kwenye kikao cha Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Philemon Sengati na Wazee wa Mkoa wa Shinyanga leo Alhamis Juni 17,2021 katik ukumbi wa CCM mkoa wa Shinyanga
Askofu wa Kanisa la EAGT Ushirika Shinyanga Raphael Machimu akiongoza maombi kwenye kikao cha Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Philemon Sengati na Wazee wa Mkoa wa Shinyanga leo Alhamis Juni 17,2021 katik ukumbi wa CCM mkoa wa Shinyanga
Kaimu Mganga Mkuu wa mkoa wa Shinyanga, Timothy Sosoma akizungumza kwenye kikao cha Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Philemon Sengati na Wazee wa Mkoa wa Shinyanga leo Alhamis Juni 17,2021 katik ukumbi wa CCM mkoa wa Shinyanga
Kikao kikiendelea
Mzee Alley Juma akizungumza kwenye kikao cha Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Philemon Sengati na Wazee wa Mkoa wa Shinyanga leo Alhamis Juni 17,2021 katik ukumbi wa CCM mkoa wa Shinyanga
Mzee Mohamed Kabale akizungumza kwenye kikao cha Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Philemon Sengati na Wazee wa Mkoa wa Shinyanga leo Alhamis Juni 17,2021 katik ukumbi wa CCM mkoa wa Shinyanga
Mzee Hashim Mkarambati akizungumza kwenye kikao cha Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Philemon Sengati na Wazee wa Mkoa wa Shinyanga leo Alhamis Juni 17,2021 katik ukumbi wa CCM mkoa wa Shinyanga
Bi. Suzana Mbalu akizungumza kwenye kikao cha Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Philemon Sengati na Wazee wa Mkoa wa Shinyanga leo Alhamis Juni 17,2021 katik ukumbi wa CCM mkoa wa Shinyanga



Picha zote na Kadama Malunde -Malunde 1 blog


Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464