Rais wa TFF Wallace Karia
Jina la Rais wa sasa wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) anaetetea nafasi yake kwenye Uchaguzi Mkuu, Wallace Karia ndio mgombea pekee aliyepitishwa na kamati ya Uchaguazi ya shirikisho hilo, miongoni mwa majaina matatu ya wagombea wa nafasi hiyo baada ya zoezi la usaili kukamilika, Kamati yaUchaguzi imethibitisha.
Wallace Karia ambae ndio Rais wa sasa wa TFF jina lake pekee ndio lilopitishwa na kamati ya uchaguzi, baada ya wagombea wengine wa nafasi hiyo ya Urais, Hawa Mniga pamoja na Evance Mgeusa kukosa vigezo vinavyokidhi kwa wao kuendelea na hatua inayofata kwenye uchaguzi.
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya TFF, Benjamini Kalume amesema kwa sasa kitakachofanyika ni Wallace Karia akiwa kama mgombea pekee ni kwenda kuthibitishwa na Mkutano mkuu na si kumpigia Kura.
Mkutano Mkuu wa TFF utafanyika Agosti 7, 2021. Mkoani Tanga ambapo moja ya Ajenda ya mkutano huo ni Uchaguzi wa kuchagua viongozi wa shirikisho hilo ikiwemo nafasi ya Urais na nafasi sita (6) za wajumbe wa kamati ya Utendaji.