MAONESHO YA PILI YA BIASHARA NA TEKNOLOJIA YA MADINI SHINYANGA KUFANYIKA JULAI 23 HADI AGOSTI 1,2021

Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga Bi. Zuwena Omary akifungua kikao cha Maandalizi ya Maonesho ya Pili ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga leo Julai 15,2021 katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga Bi. Zuwena Omary akifungua kikao cha Maandalizi ya Maonesho ya Pili ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga leo Julai 15,2021 katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga. 

Katibu wa Kamati ya Maonesho  Mhandisi Joseph Kumburu  ambaye ni Afisa Madini Mkazi Mkoa wa Shinyanga akitoa taarifa kwenye kikao cha Maandalizi ya Maonesho ya Pili ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga yanayotarajia kufanyika kuanzia Julai 23,2021 hadi Agosti 1,2021 katika uwanja wa kijiji cha Butulwa kata ya Old Shinyanga Manispaa ya Shinyanga.
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akizungumza kwenye kikao cha Maandalizi ya Maonesho ya Pili ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga yanayotarajia kufanyika kuanzia Julai 23,2021 hadi Agosti 1,2021 katika kijiji cha Butulwa kata ya Old Shinyanga Manispaa ya Shinyanga.

Mwenyekiti wa Kamati ya Maonesho, Dkt. Kulwa Meshack ambaye pia ni Mwenyekiti wa TCCIA mkoa wa Shinyanga akizungumza kwenye kikao cha Maandalizi ya Maonesho ya Pili ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga yanayotarajia kufanyika kuanzia Julai 23,2021 hadi Agosti 1,2021 katika kijiji cha Butulwa kata ya Old Shinyanga Manispaa ya Shinyanga.
Mwenyekiti wa Kamati ya Maonesho, Dkt. Kulwa Meshack ambaye pia ni Mwenyekiti wa TCCIA mkoa wa Shinyanga akizungumza kwenye kikao cha Maandalizi ya Maonesho ya Pili ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga 
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga, Mhe. David Nkulila akizungumza kwenye kikao cha Maandalizi ya Maonesho ya Pili ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyangayanayotarajia kufanyika kuanzia Julai 23,2021 hadi Agosti 1,2021 katika kijiji cha Butulwa kata ya Old Shinyanga Manispaa ya Shinyanga.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga Bi. Zuwena Omary (kulia) akiteta jambo na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Jasinta Mboneko kwenye kikao cha Maandalizi ya Maonesho ya Pili ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga.
Wadau wakiwa kwenye kikao cha Maandalizi ya Maonesho ya Pili ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga.

Mwenyekiti wa Kamati ya Maonesho, Dkt. Kulwa Meshack ambaye pia ni Mwenyekiti wa TCCIA mkoa wa Shinyanga (kushoto) akiteta jambo na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga, Mhe. David Nkulila. 
Wadau wakiwa kwenye kikao cha Maandalizi ya Maonesho ya Pili ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga.
Wadau wakiwa kwenye kikao cha Maandalizi ya Maonesho ya Pili ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga.
Wadau wakiwa kwenye kikao cha Maandalizi ya Maonesho ya Pili ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga.
Wadau wakiwa kwenye kikao cha Maandalizi ya Maonesho ya Pili ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga.
Wajumbe wa Sekretarieti ya Mkoa wa Shinyanga wakiwa kwenye kikao cha Maandalizi ya Maonesho ya Pili ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga
Wadau wakiwa kwenye kikao cha Maandalizi ya Maonesho ya Pili ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga
Wadau wakiwa kwenye kikao cha Maandalizi ya Maonesho ya Pili ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mkoa wa Shinyanga umeandaa Maonesho ya Pili ya Biashara na Teknolojia ya Madini yanayotarajia kufanyika kuanzia Julai 23,2021 hadi Agosti 1,2021 katika uwanja wa kijiji cha Butulwa kata ya Old Shinyanga Manispaa ya Shinyanga.

Akizungumza katika kikao cha Maandalizi ya Maonesho ya Pili ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga leo Alhamisi Julai 15,2021, Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga Bi. Zuwena Omary amesema maonesho hayo yanalenga kufungua fursa mbalimbali za biashara na kukuza uwekezaji.

"Tunawakaribisha wafanyabiashara, wajasiriamali na wadau mbalimbali kushiriki katika Maonesho haya ambayo yatasaidia kutangaza mkoa wa Shinyanga na kukuza uwekezaji. Shinyanga tuna fursa nyingi za kiuchumi, tunatamani siku moja Maonesho ya Biashara na Teknolojia ya Madini Kitaifa yafanyike mkoani Shinyanga",amesema Omary.

Akitoa taarifa kwenye Kikao cha Maandalizi ya Maonesho ya Pili ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga leo Julai 15,2021, Katibu wa Kamati ya Maonesho  Mhandisi Joseph Kumburu  ambaye ni Afisa Madini Mkazi Mkoa wa Shinyanga amesema malengo makuu ni kukuza biashara, viwanda na madini ili kujenga uchumi jumuishi na fungamishi.

“Maonesho haya yanafanyika kwa ushirikiano wa Sekta ya Umma na Sekta Binafsi. Sekta ya Umma inaongozwa na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga na Sekta inaongozwa na Chemba ya Biashara, Viwanda na Kilimo (TCCIA) Mkoa wa Shinyanga”,amesema Mhandisi Kumburu.

Ameyataja baadhi ya malengo ya maonesho hayo kuwa ni pamoja na kutoa fursa kwa wafanyabiashara wa ndani na nje ya nchi na taasisi mbalimbali kukutana na wanunuzi kwa lengo la kutangaza bidhaa na huduma wanazotoa, kujifunza masuala ya biashara na teknolojia ya madini kulingana na soko la kimataifa na mifumo ya usambazaji madini katika masoko mbalimbali.

“Malengo mengine ni kutengeneza mitandao ya mawasiliano ya kibiashara na teknolojia ya madini miongoni mwao ili iwasaidie kukuza biashara,kutangaza fursa za uwekezaji zilizopo Shinyanga na kukutanisha wadau wa viwanda, biashara na madini ili kubadilishana uzoefu ili kukuza shughuli zao”,ameongeza Mhandisi Kumburu.

Kwa upande wake, Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko amewahamasisha wafanyabiashara na wajasiriamali kushiriki katika maonesho hayo huku akiwataka kuchukua tahadhari juu ya ugonjwa wa Corona kwa kuhakikisha wanavaa barakoa, kunawa mikono kwa maji tiririka na sabuni na kutumia vitakasa mikono 'Sanitizer'.

Naye Meya wa Manispaa ya Shinyanga Mhe. David Nkulila na Mwenyekiti wa Kamati ya Maonesho, Dkt. Kulwa Meshack ambaye pia ni Mwenyekiti wa TCCIA mkoa wa Shinyanga wamesema mafanikio ya Maonesho hayo yatatokana na ushiriki wa wadau hivyo kuwataka wadau wote kushiriki kikamilifu.

Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464