Muonekano wa Soko la Kariakoo Jijini Dar es salaam
JESHI LA ZIMAMOTO LATAJA SABABU KUCHELEWA KUZIMWA MOTO SOKO LA KARIAKOO
JESHI LA ZIMAMOTO LATAJA SABABU KUCHELEWA KUZIMWA MOTO SOKO LA KARIAKOO
WAKATI Serikali ikiwataka wakuu wote wa mikoa kufanya ukaguzi katika maeneo yote ya soko na vituo vya mabasi nchini, Jeshi la Zimamoto na Ukoaji limetoa sababu tano zilizofanya kuchelewa kuzima moto katika Soko Kuu la Kariakoo Jijini Dar es salaam ,huku msongamano wa vibanda ukitajwa.
Hayo yameelezwa jana na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dar es Salaam, Kamishna Msaidizi Bakari Kassa Mrisho, akimuelezea Waziri wa Mambo ya Ndani, George Simbachawene,changamoto walizopata wakati wa zoezi la uzimaji moto ndani ya soko hilo la Kariakoo.
Alisema changamoto kubwa ni miundombinu ya soko la Kariakoo kuwa na msongamano mkubwa na kuzungukwa na vibanda ambavyo haviruhusu magari kuingia na kutoka kwa haraka.
Alitaja changamoto ya visima vya maji ambavyo katika maeneo ya jirani ikiwemo na kilichopo Mtaa wa Nyati Kariakoo vimeziba matope na kufanya presha ya maji kuwa ndogo hivyo kuwalazimu kufuata maji maeneo ya uwanja wa ndege.
Tatu alisema kuwa changamoto nyingine ni uelewa wa wananchi kwenye majanga, ambapo katika tukio hilo la moto wananchi walikimbilia eneo la tukio badala ya kukimbia mbali na eneo la janga hilo.
Pia vibaka nao wametajwa kama changamoto ambao walikuwa wakikimbilia eneo la tukio na kuiba bidhaa za watu na kwamba Polisi wa usalama walikuwa wachache.
Muundo wa jengo la soko la Kariakoo ni wa kizamani hauna ving’amuzi moto ambavyo kukiwa na tukio lolote la hatari vinapiga alamu na hatua za haraka zinachukuliwa.
WAZIRI AELEKEZA WAKUU WA MIKOA

Kufuatia changamoto hizo, Waziri Simbachawene ameagiza wakuu wote wa mikoa kushirikiana na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kufanya ukaguzi katika maeneo yote yenye mikusanyiko ikiwemo masoko, vituo vya mabasi, viwanja vya mpira na maeneo mengine yote yenye mikusanyiko ya watu, ili kubaini yenye dosari kwa ajili ya kudhibiti majanga.
“Tunafikiria namna ya kulipanga soko hili kwa namna nzuri, maeneo haya lazima yawe na maji yenye presha kubwa, kukosekana kwa ‘fire hydrant’ ndio pelekea madhara haya makubwa.
“Miundombinu ina ‘discourage’ majanga ya moto yanavyotokea, pia jengo ni la zamani, linatakiwa kuwekwa vifaa vya kisasa vya kuditect moto na kutoa alarm, kuna maeneo mengi yanachangamoto nyingi.
“Nawaagiza wakuu wote wa Mikoa nchi nzima, watumie Jeshi la Zimamoto kupita maeneo yote ya umma, masoko, stendi na maeneo yote yanayokusanya moto lazima tuhakikishe tunayalinda majanga yanapotokea.
“Sina hakika kwenye stendi na masoko kama kuna miundombinu ya namna hiyo, majanga manne kwa siku moja yametoea juzi, majanga mawili Morogoro, changamoto ni zile zile, hakuna chanzo cha kuzima moto, silaha ya kuzima moto ni maji kama hakuna ‘hydrant’ madhara ndio kama haya, majengo yote makbuwa yakaguliwe, tukio la Kariakoo liwe mfano, Barabara ya Ali Hassan Mwinyi kwenda Mwenge kuna majengo mazuri sana lakini sina hakika kama kuna ‘fire hydrant’.
“Simamieni , tokeni mseme changamoto zilizopo kwa uwazi na maeneo gani yanapaswa kuboreshwa, msiposema sasa mtaonekana watu wa ajabu,” Simbachawene aliliambia Jeshi la Zimamoto.
Kwa upande wa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla, alisema tangu siku ya kwanza tukio la moto lilivyotokea alikuwa eneo la tukio na kujionea changamoto kubwa namna magari ya Zimamoto yanavyoingia na kutoka ilikua ni shida, ndio maana zoezi la kudhibiti moto usiende nyumba za jirani, soko dogo, kunusuru benki limechukua muda mrefu.
“Changamoto zote zilizoelezwa na zimamoto tutazifanyia kazi, ni lazima tufanye maamuzi magumu, hadi sasa zoezi la kuzima moto linaendelea tunashukuru tu tumefanikiwa kuudhibiti kwa kiasi kikubwa, shimoni wafanyabiashara 397 hawajaathirika, vibanda 99 pia havijaathirika, kulikoathirika ni huko juu na hapa ghorofa ya kwanza wafanyabiashara 224 ndio wameathirika, tunaendelea na uhakiki,” alisema Makala na kuongeza;
Aidha Makalla alimeziagiza Mamlaka ya Mamlaka ya Dawa, Vitendanishi na Vifaa Tiba (TMDA) Shirika la Viwango. Tanzania (TBS), na Ofisi ya Mkemia Mkuu kufika soko la Kariakoo na kuthibiti ubora wa bidhaa kwa kile alichoeleza kuwa maji ya zimamoto yana kemikali na pia kuna viutailifu ambavyo vimelipuka, hivyo bidhaa lazima zithibitishwe kama ni salama kuendelea kutumiwa na binadamu.
Na Vicky Kimaro; Chanzo Habari Leo.