KATAMBI AUNGURUMA KOLANDOTO, AGUSIA MACHINJIO YA KISASA


Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobas Katambi, ambaye pia Naibu Waziri wa Nchi Ofisi wa Waziri Mkuu Kazi, Vijana, na Ajira, akizungumza na wananchi kwenye mkutano wa hadhara Kolandoto.



Na Marco Maduhu, Shinyanga.


Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobas Katambi, ambaye pia Naibu Waziri wa Nchi Ofisi wa Waziri Mkuu Kazi, Vijana, na Ajira, amefanya mkutano wa hadhara Kata ya Kolandoto kusikiza kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.


Akizungumza na wananchi wa Kata hiyo leo kwenye mkutano wa hadhara, amesema amejipanga vyema kutekeleza ahadi zake kwa vitendo ambazo aliziahidi kwenye kipindi cha kampeni 2020.

Amesema kwenye Kata hiyo kuna changamoto mbalimbali ambazo amezisikia kutoka kwa wananchi, ikiwamo ya ujenzi wa miundombinu ya barabara, maji, umeme, afya, upimaji wa ardhi, pamoja na ucheleweshwaji wa malipo ya Penshine za wazee.

"Mimi sina siasa za porojo, siasa zangu ni kazi tu, nazani matunda mmeanza kuona ndani ya kipindi changu kifupi, na hadi kufikia miaka mitano, Shinyanga itakuwa na maendeleo makubwa," amesema Katambi.

"Sasa hivi tumeshatoka kwenye mchakato wa bajeti, na fedha nyingi tu zimeshatengwa kwa ajili ya utekelezaji wa maendeleo ya wananchi, ambapo katika Bajeti ya barabara kuna Sh. bilioni 1.5 zitatumika kwa barabara za ndani tu, tumpongeze Rais wetu Samia," ameongeza Katambi.

Aidha amesema katika utendaji wake wa Kazi, hata ogopa mtu yoyote, na ata hakikisha mradi wa machinjio ya mifugo ya kisasa ambayo ipo Ndembezi, ina kamilika na kuanza kufanya kazi.

Naye Katibu wa CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini Agnes Bashemu, amempongeza Mbunge Katambi, kwa kufanya kazi kwa vitendo, pamoja na kuitendea haki Wizara ambayo ameteuliwa na Rais Samia.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga, Salu Ndogo, ambaye ni Afisa mipango miji na Mkuu wa idara ya ardhi, amesema wamejipanga vyema kutatua changamoto zote za wananchi.

Pia amesema kwenye Kata hiyo ya Kolandoto watafika mwezi September kupima ardhi na kurasimisha, hali ambayo itasaidia kutatua migogoro ya ardhi na kuwataka wananchi waendelee kulipia gharama za upimaji wa ardhi zao.

Mbunge Katambi ameanza ziara yake leo Jimboni mwake kwa ajili ya kuzindua miradi ya maendeleo ukiwamo ujenzi wa kisima cha maji Shule ya Sekondari Kolandoto na Daraja la Uzogore- Bugwandege, pamoja na kusikiliza kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.

TAZAMA PICHA HAPA CHINI


Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobas Katambi, ambaye pia Naibu Waziri wa Nchi Ofisi wa Waziri Mkuu Kazi, Vijana, na Ajira, akizungumza na wananchi kwenye mkutano wa hadhara Kolandoto.

Katibu wa CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini Agnes Bashemu, akizungumza kwenye mkutano wa hadhara na Wananchi wa Kolandoto.

Diwani wa Kolandoto Mussa Andrew, akizungumza kwenye mkutano huo.

Mtendaji wa Kolandoto Wilison Mwakaluba, akizungumza kwenye mkutano huo.

Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga Salu Ndogo, ambaye ni Afisa Mipango Miji na Mkuu wa Idara ya Ardhi, akizungumza kwenye mkutano huo.

Afisa maendeleo Manispaa ya hinyanga John Tesha, akizungumza kwenye mkutano huo.

Kaimu Mganga Mkuu wa Manispaa ya Shinyanga Charles Malogi, akizungumza kwenye mkutano huo.

Kaimu Mkurugenzi wa mamlaka ya maji na usafi wa mazingira mjini Shinyanga (SHUWASA), Masaka Kambesha, akizungumza kwenye mkutano huo.

Viongozi wa CCM wakiwa kwenye mkutano huo.

Baadhi ya Wananchi wa Kolandoto wakiwa kwenye mkutano wa hadhara.

Mmoja wa Wananchi wa Kolandoto akinawa kwa Sabuni na Majitiririka kwa ajili ya kujikinga na Corona kwenye mkutano huo wa hadhara.

Baadhi ya Wananchi wa Kolandoto wakiwa kwenye mkutano wa hadhara.

Baadhi ya Wananchi wa Kolandoto wakiwa kwenye mkutano wa hadhara.

Na Marco Maduhu- Shinyanga.












































Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464