KIONGOZI MBIO ZA MWENGE WA UHURU AWEKA JIWE LA MSINGI MRADI KUWAJENGEA UWEZO WAKULIMA KAHAMA


Kiongozi wa Mbio Maalum za Mwenge wa Uhuru Luten Josephine Mwambashi, akiweka jiwe la Msingi kwenye mradi wa kuwajengea uwezo wakulima Manispaa ya Kahama.


Suzy Luhende, Kahama


Kiongozi wa Mbio Maluum za Mwenge wa Uhuru Luten Josephine Mwambashi, ameweka jiwe la msingi katika mradi wa kuwajengea uwezo wakulima Manspaa ya Kahama, na kuongeza tija katika uzalishaji na upatikanaji wa masoko ya mazao.
 
Mradi huo umewekewa jiwe la msingi jana katika Kata za Mondo na Mwendakulima Manispaa ya Kahama, uliofadhiliwa na kampuni za uchimbaji madini ya dhahabu PANGEA na BUZWAGI, ambao utasaidia kuwajengea uwezo wakulima, ili kuongeza tija katika uzalishaji na upatikanaji wa masoko ya mazao ambao utagharimu zaidi ya Sh. milioni 500.

Akisoma Risala mbele ya kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru Meneja wa mradi huo Eribariki Jambau, aalisema mradi huo utakuwa ni kituo cha kupatikana maarifa ya kilimo kwa wakulima wa Manispaa ya Kahama.

"Mpaka sasa kazi zilizokamilika ni upandaji miti ya mbao, ubebeshaji wa miche ya matunda, ujenzi wa kitalu nyumba, ujenzi wa kisiwa cha maji ununuzi wa Trekta, Mashine ya kupukuchua mahindi, mpunga, na kwenye miti ya matunda"alisema Jambua.

Jambua alitaja vitu vingine kuwa ni mashine ya kupima unyevu, uzito, pamoja na kutoa mafunzo kupitia mashamba ya mfano kwa wakulima 1,801, sawa na asilimia 46.8 na wakulima waliolengwa ni 3,924 ,na shughuli hizo zimegharimu kiasi cha Sh 138,763,285,00.

Amesema kupitia mradi huo pia vijana 200 watajengewa uwezo wa kilimo biashara, na wataimarisha AMCOS mbili, na kuimalisha vikundi vya uzalishaji mali 29.

Kwa upande wake Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Luten Josephine Mwambashi, amewashauri wausimamie vizuri mradi huo ili uweze kuwasaidia wakulima kupata mazao mengi, na kuweza kujikwamua kiuchumi.

"Mradi huu tumeukagua ni mradi mzuri, kwa sababu wakulima watafaidika nao, hivyo tunauwekea jiwe la msingi , lakini naomba muusimamie vizuri ili uwe mradi endelevu waukute vizazi na vizazi, alisema ,"Mwambashi.

Baadhi ya wananchi wa Kata ya Mondo Bakari Salumu na Thereza Mwandu walizishukuru kampuni hizo za uchimbaji madini ya dhahabu, kwa kuwawekea mradi huo kwani watafaidika kwa kujifunza kilimo cha kisasa na chenye tija, ili waweze kujipatia kipato na kuinuka kiuchumi.


Kiongozi wa Mbio Maalum za Mwenge wa Uhuru Luten Josephine Mwambashi akiweka jiwe la Msingi  kwenye mradi wa kuwajengea uwezo wakulima Manispaa ya Kahama.



Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464