MWANAMKE AKUTWA MTUPU AKIWA AMEUAWA SHINYANGA



Wakazi wa Majengo Manispaa ya Shinyanga, wakiangalia mwili wa Marehemu Lucia Michael maarufu mama Kulwa, ambaye ameuawa na watu wasiojulikana.



Na Marco Maduhu, Shinyanga

Mwanamke Lucia Michael maarufu Mama Kulwa, mkazi wa Majengo Manispaa ya Shinyanga, amekutwa ameuwa na watu wasiojulikana, na mwili wake kutupwa nyuma ya msikiti wa Majengo.

Tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia leo, ambapo aligundulika na majirani majira ya saa 12 asubuhi, mara baada ya kuuona mwili wake ukiwa nyuma ya msikiti wa majengo jirani na makazi yao akiwa mtupu.

Akielezea tukio hilo mmoja wa majirani Anastazia Amosi, alisema baada ya kupata taarifa, alifika eneo la tukio na kumkuta jirani yake akiwa mtupu huku amuawa, ndipo wakamfunika nguo na kutoa taarifa kwa Mwenyekiti wa mtaa.

"Mwanamke huyu ni jirani yetu ana watoto watatu, na kazi yake ni msusi maarufu sana hapa mtaani kwetu, tunasikitika sana kumkuta akiwa ameuawa tena kavuliwa nguo zote," alisema Amosi.

Naye Mwenyekiti wa Majengo Manispaa ya Shinyanga Iddi Bwana, alisema mwanamke huyo huenda aliuawa na vibaka, na kisha mwili wake kutupwa nyuma ya Msikiti jirani na makazi ya watu.

Kwa upande wake Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga George Kyando, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo, na kubainisha kuwa Jeshi bado linafanya uchunguzi ili kubaini chanzo chake na wahusika

TAZAMA TUKIO LA PICHA HAPA CHINI


Wakazi wa Majengo Manispaa ya Shinyanga, wakiangalia mwili wa Marehemu Lucia Michael maarufu mama Kulwa, ambaye ameuawa na watu wasiojulikana.

Jeshi la Polisi likiuchukua Mwili wa Marehemu Lucia Michael.

Na Marco Maduhu- Shinyanga.































Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464