Tanki la kuhifadhia maji katika mradi wa maji Kata ya Bubiki wilayani Kishapu ambao umezinduliwa na Mbio za Mwenge wa Uhuru.
Na Suzy Luhende, Kishapu.
Kiongozi wa Mbio Maluum za Mwenge wa uhuru Luten Josephine Mwambashi, amezindua mradi wa maji wa kisima kirefu katika Kata ya Bubiki Halmashauri ya wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga, utakao wanufaisha wananchi zaidi ya 50,00 sawa na asilimia 91.
Luten Mwambashi amezindua kisima hicho Julai 10 mwaka huu wakati wa Mbio za Mwenge wa Uhuru wilayani Kishapu.
Aidha amewataka wananchi wautunze mradi huo pamoja na miundombinu yake kwa kuto iharibu ili udumu kwa muda mrefu kuwapatia maji safi na salama, na kuondokana na adha ya kutumia maji yasiyofaa kiafya.
“Kwenye maelezo ya mdomo tumeeleza mradi huu umetumia kiasi cha fedha Sh, milioni 312.6, huku kwenye katarasi kikielezwa kutumika kiasi cha Sh ,milioni 311 ambapo kimesalia kiasi cha Sh 890,000, hivyo na shauri fedha hizi zitumike kutengeneza maeneo madogomadogo yaliyobaki ili wananchi waweze kunufaika na usiharibike mapema”alisema Luten Mwambashi.
Kwa upande wake Kaimu Meneja wa wakala wa maji vijijini (Ruwasa) wilayani Kishapu Dickson Kamazina, alisema mradi huo wa maji unanufaisha wakazi zaidi ya 5,000 sawa na asilimia 91 kutoka vijiji vya Bubiki A na Bubiki B, na kuna vituo nane vya kuchotea maji (DP) na ulichukua muda wa miezi kumi kukamilika kwake.
Baadhi ya wananchi wa kijiji hicho Luhende Kulwa na Monika Mboje, walisema hawana tena shida ya maji, na kuipongeza Serikali kwa kuwajali wananchi wake, ambapo walidai ni miaka mingi walikuwa wakitumia maji ya madimbwi ambayo siyo salama kiafya..
TAZAMA PICHA HAPA CHINI

Kiongozi wa Mbio Maalum za Mwenge wa Uhuru Luten Josephine Mwambashi, akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi wa maji Kata ya Bubiki wilayani Kishapu,kuli ni Mbunge wa Jimbo la Kishapu Boniphace Butondo na kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Kishapu Jonas Mkude.
Mhandisi wa maji wilaya ya Kishapu Dickson Kamazina, akitoa maelekezo ya mradi wa maji Kata ya Bubiki, kwa Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Josephine Mwambashi ambao utanufaisha Wananchi wa vijiji viwili, Bubiki A na Bubiki B.
Tanki la kuhifadhi maji lenye ujazo wa Lita 100,000, ambalo litafaidisha Wakazi zaidi ya 50,00 wa kijiji Cha BubikI wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga.