ELIMU KWA UMMA KUHUSU USAJILI NA WA NAMBA YA SİMU NA UHALIFU
KWA NAMBA 106
1. Historia
ya usajili.
Usajili wa laini za simu ni zoezi la
awali kabisa ambalo hufanyika mtu anaponunua laini yake ya simu ambapo mtumiaji
hutakiwa kukamilisha umiliki wa laini yake kwa kuweka namba yake ya
kitambulisho cha taifa ambayo itahibitisha kwa kutumia alama zake za vidole.
Usajili wa laini ni utekelezaji wa Sheria
ya Mawasiliano ya Kieletroniki na Posta (EPOCA) ya 2010 na Kanuni ya
Mawasiliano ya Kielektroniki ya Posta (Usaili wa laini za simu ya simu) ya 2018
ambazo zinamtaka pamoja na mambo mengine mtu yoyote anayetaka kutumia laini ya
simu ahakikishe kuwa anaisajili namba hiyo kwa kutumia namba yake ya
kitambulisho cha taifa.
2. Kwanini
tunahakiki?
Baada ya kukamilika kwa zoezi la usajili
wa laini kulionekana mapungufu ambapo baadhi ya watu kwa kujua na wengine kwa
kutojua waliwasajilia watu wengine laini zao jambo ambalo ni kinyume cha
sheria.
Zoezi la uhakiki limekuja kurekebisha
mapungufu hayo ambapo sasa mtumiaji amejengewa uwezo wa kuweza kuangalia ni
namba ngapi zimesajiliwa kwa kutumia namba yake ya kitambulisho cha taifa na
iwapo atakuta namba ambazo hazifahamu anaweza kuzitoa.
3. Tofauti
ya kusajili na kuhakiki.
Tofauti ya usajili na uhakiki ni kwamba
usajili ni zoezi la awali kabisa ambalo hufanyika mtu anamponunua laini yake ya
simu ambapo mtumiaji hutakiwa kukamilisha umiliki wa laini yake kwa kuweka
namba yake ya kitambulisho cha taifa ambayo itathibitisha kwa kutumia alama
zake za vidole.
Uhakiki ni hatua ambayo mwananchi
anaifanya kujiridhisha iwapo usajili wake umekamilika na pia kuweza kutambua
namba za simu ambazo zimesajiliwa kwa kutumia namba yake ya kitambulisho cha
taifa.
4. Utaratibu
wa kuhakiki ukoje? (kutakuwa na foleni kama ilivyokuwa kusajili?
Utaratibu wa kuhakiki ni mwepesi sana
unachotakiwa kufanya ni kubonyesha *106# alafu kufuata maelekezo. Uhakiki
hufanyika kwa kutumia simu yako ya mkononi hivyo hakutakuwa na haja ya kwenda
kupanga foleni kuhakiki. Wakati pekee ambao utatakiwa kwenda kwa mtoa huduma ni
pale ambapo umehakiki na kukuta namba ambayo huitambui na unataka kuitoa, hapo
ndipo utatakiwa kwenda kwa mtoa huduma akusaidie kuitoa.
5. Uhakiki
utasaidiaje kupunguza uhalifu?
Wahalifu wanatumia namba ambazo
zimesajiliwa na watu wengine kufanyia uhalifu hivyo iwapo utahakiki namba zako
na ukatoa namba zote ambazo huzifahamu lakini zimesajiliwa kwa kutumia namba ya
kitambulisho chako basi utakuwa umewezesha kuzuia uhalifu maana namba hizo
zitazimwa.
6. Je
ni kosa kutumia laini ambayo haijasajiliwa kwa kutumia jina na namba ya
kitambulisho chako cha taifa?
Ndio, Sheria ya Mawasiliano ya
Kieletroniki na Posta (EPOCA) ya 2010 na Kanuni ya Mawasiliano ya Kielektroniki
ya Posta (Usaili wa laini za simu ya simu) ya 2018 zinakataza kutumia laini
ambayo haijasajiliwa kwa kutumia jina na namba yako ya kitambulisho cha taifa
na endapo utabainika kufanya hivyo hatua za kisheria zitachukuliwa kwa wewe
unayetumia na aliyetoa namba yake isajili namba ambayo haitumii yeye.
7. Mamlaka
inawataka wananchi wafanye nini?
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania inawataka
watumiaji wote wa huduma za simu kuhakikisha kuwa wanatumia laini ambazo
zimesajiliwa kwa kutumia namba zao za vitambulisho vya taifa na wajenge
utaratibu wa kuhakiki namba hizo kwa kuhakikisha kuwa anazitambua na kuridhia
namba zote ambazo zimesajiliwa kwa kutumia kitambulisho chake cha taifa.
Na iwapo atakuta namba ambayo haitambui
basi aende kwa mtoa huduma ili waitoe namba hiyo katika orodha ya namba ambazo
anazimilikiwa kwa kutumia kitambulisho chake.
8. Uhakiki
wa simu unasaidiaje unapopotelewa na simu?
Uhakiki wa simu
unakusaidia kuwa salama unapotumia huduma zako za simu. Unapopotelewa na simu
hatua unazotakiwa kufuata ni kutoa taarifa polisi na kisha kwa mtoa huduma wako
ili namba hiyo iweze kuzimwa na baadae uweze kupatiwa laini nyingine ya simu
ambayo itakuwezesha kuendelea kutumia huduma za mawasiliano kama ilivyoawali.
KWA NAMBA 15040
1.
Namba hii ni ya nini?
Hii ni namba ya huduma ambayo imetolewa
na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzanani kwa watoa huduma ili waweze kuitumia kupokea
taarifa za namba ambazo zinatumika katika uhalifu.
2
2.
Namba hii iko wapi?
Namba hii iko kwa watoa huduma wote.
3.
15040 inafanyaje kazi?
Namba ya huduma ya 15040 imeunganishwa
moja kwa moja na mtoa huduma hivyo mtumiaji anapotuma namba iliyofanya uhalifu
kwenda kwenye namba hii mtoa huduma huipokea na kuifanyia kazi namba hiyo
ambapo baadhi ya hatua ambazo huchukuliwa ni kuiripoti namba hiyo kwa mamlaka
zinazohusika na kukabiliana na uhalifu na kisha kuifunga namba hiyo.
4.
Je namba hii inalipiwa?
Hapana, huduma kwenda kwenye namba hii ni
bure. Hata hivyo kwa wale ambao wanatumia simu janja ambazo zinatumia mfumo wa
Andriod wanapotumia huduma hii wataulizwa iwapo wako tayari kuilipia ambapo
mtumiaji atatakiwa kukubali kulipia ndipo ujumbe uende japo kiuhalisia hatokatwa
malipo yoyote.