Na Mwandishi Wetu, Shinyanga
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa kodi Kahama kwa mwaka wa fedha 2020/2021 Julai mwaka jana hadi Juni 30 mwaka huu ilipangiwa kukusanya Sh. Bilioni 18.532 na ilifanikiwa kukusanya Sh. Bilioni 40.042 ambayo ni sawa na asilimia 227.
Taarifahiyo ilitolewa na Kaimu Meneja wa TRA Mkoa wa kodi Kahama, Irene Donard Hance wakati akizungumza na Shinyanga Press Club Blog juu ya namna walivyo fanikiwa kukusanya mapato juu ya kiwango walicho pangiwa
kwa mwaka wafedha 2020,2021 ambapo walifanikiwa kukusanya jumla ya Shilingi Milioni 40.042 sawa na asilimia 227.
Irine Hance akiwa kwenye shughuli zake
Airene alisema kuwa miongoni mwa mikakati iliyo wasaidia kwa kiasi kikubwa kufanikiwa kukusanya kiasi hicho ni pamoja na mikakati mbalimbali waliyoweka ikiwemo kuwafikia wafanyabiashara na kuwapa elimu ya
ulimapi kuodi kwa hiari hali iliyo wafanya wafanyabiashara wengi kujitokeza na kuunga mkono jitihada za serikali kwa kuhakikisha wanalipa kodi kwa maendeleo ya Taifa.
"Mwaka wafedha ulio malizika kuanzia Julai Mosi 2020 hadi Juni 30 tumekusanya Sh. Bilioni 40.0429 sawa na asilimia 227 ya lengo la makusanyo hivyo natumia nafasi hii kuwaomba na kuwakumbusha wafanyabiashara na walipa kodi kwa ujumla kutimiza wajibu wao kwa kuwndelea kulipa kodi ili mkoa wakikodi Kahama uendelee kufanya vizuri
katika ukusanyaji wa mapato," alisema Airene.
"Jukumu la Mamlaka ya mapato ni kukusanya mapato ya serikali ili uchumi wa nchi uzidi kuimarika,niwajibu wetu kutoa elimu kwa walipa kodi na Watanzania kwa ujumla pamoja na kutoa huduma bora ili kuongezea lidhaa ya hiari ya ulipaji kodi na kupanua wigo wa upatikanaji wa mapato", aliongeza Airene.
Aidha Airene aliwataka wafanyabiashara wa mkoa wa kodi Kahama kutoa risiti pindi wanapo fanya biashara zao pamoja na wafanya biashara kudai risiti pindi wanapo nunua bidhaa kutoka kwa wafanyabiashara ili kutimiza matakwa ya kisheria yanayo mtaka kila muuzaji kutoa risiti na mununuzi kudai risiti huku akiahidi kuendele kutoa elimu ya ulipaji
kodi kwa wananchi.
Nao baadhi ya wafanyabiashara waliozungumza na Shinyanga Press Club Blog wameupongeza uongozi wa mkoa wa kikodi Kahama kwa kuvuka lengo la makusanyo na kuahidi kuendelea kuunga mkono serikali kwa kulipa kodi
ili seerikali iweze kukamilisha miradi mbalimbali ya maendeleo inayo tekelezwa na serikali ya awamu ya sita.
"Taifa imara linatokana na uchumi imara hivyo tutakuwa wazalendo katika ulipaji wa kodi na kwakufanya hivyo itatusaidia kufanya kazi zetu kwa uhuru na amani", walisema wafanyabiasara.
Wafanyakazi wa TRA mkoa wa Kahama wakiwa katika picha ya pamoja