SOMA VIGEZO VYA MAOMBI YA RUZUKU HAPA CHINI👇👇👇
I. UTANGULIZI
The registered Trustee of Women Fund Tanzania (WFT-Trust) ni mfuko unaotoa ruzuku kwa maswala ya haki za wanawake uliosajiliwa mnamo 2008 kama shirika lisilo la kiserikali, mnamo Septemba 2019 ilisajiliwa upya kama Wadhamini waliosajiliwa wa Mfuko wa Wanawake Tanzania. Mfuko unazingatia kusaidia utekelezaji wa miradi ambayo inalenga kukuza upatikanaji wa haki za wanawake, wasichana na watoto na kwa kuchagiza mabadiliko chanya katika jamii kuhusu haki za wanawake ,wasichana na watoto kwa kuchangia ujenzi wa TAPO la wanawake kimapinduzi Tanzania na harakati za kuleta usawa wa kijinsia kwa kuimarisha harakati za wasichana na wanawake nchini kwa lengo la kukuza uwezo juu ya maswala na haki za wanawake, wasichana na watoto Tanzania.
Katika wito huu , WFT-Trust itatoa ruzuku kwa taasisi, mashirika ya kijamii na kiraia au vikundi vitakavyokidhi vigezo na masharti ambavyo vinatekeleza shughuli mbalimbali za kupinga ukatili dhidi ya wanawake na watoto chini ya Mpango Kazi wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto ( MTAKUWWA) katika Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.
Mashirika ya kijamii/ vikundi yenye vigezo yanakaribishwa kulete maandiko yao ya kuomba ruzuku kwa ajili ya utekelezaji wa afua zilizopo ndani ya MTAKUWWA na zinazotekelezwa ndani ya halmashauri ya wilaya ya Shinyanga kupitia michakato mbalimbali ya utekelezaji huo.Lengo kuu ya ufadhili huu ni kusaidia kutokomeza ukatili dhini ya wanawake na Watoto kwa njia shirikisha na jumuishi kama zilivyoainishwa ndani ya MTAKUWWA.
Maswala mengine yanayoweza kuombewa ruzuku ni pamoja na michakato na mikakati ya kuboresha utekelezaji wa mpango wa MTAKUWWA ndani ya halmashauri husika. Mikakati hiyo inaweza kuwa na lengo la kuongeza umiliki na uwezo wawanajamii kushiriki na kushika hatamu za utekelezaji na kujengea uwezo wa watendaji wa Serikali za Mitaa na wengine (kama vile Asasi za kijamii, Mashirika yasiyo ya Kiserikali, jamii na wadau wengine) katika muundo wa MTAKUWWA ili kuongeza ufanisi na kukuza mifumo shirikishi ili kuhakikisha ushiriki wa jamii katika utekelezaji wa MTAKUWWA.
II. WFT-TRUST INATARAJIA RUZUKU ZITAKAZOTOLEWA ZIENDE KUTEKELEZA MIKAKATI IFUATAYO.
• Kuchagiza utekelezaji wa masuala ya jamii yanayohusiana na MTAKUWWA pamoja na kuhakikisha kuwa kuna uhusiano wa moja kwa moja kati ya tatizo linaloshughulikiwa, mikakati ya utekelezaji pamoja na matokeo yanayopimika kutokana nautekelezaji wa mradi husika.
• Kuonesha uendelevu wa shughuli zilizofadhiliwa,ubunifu pamoja na jinsi ya kuonesha ni jinsi gani kuna uwezekano wa shughuli hizo kutumika kama mfano kwa maeneo mengine kwa kiwangu cha juu zaidi.
• Kuonesha mchango wake katika jitihada za ujenzi wa TAPO la pamoja baina ya watetezi wa haki za wanawake na watoto na pia katika kupigania kutokomeza aina zote za uklatili dhidi ya wanawake na watoto kwa pamoja na haswa kwa kuimarisha muingiliano baina ya mashirika na asasi hizo za utetezi.katika (harakati/ vuguvugu la pamoja) kwa lengo la kutengeneza / kuimarisha mitandao na majukwaa ya kuleta nguvu ya pamoja
• Kujenga ari ya umiliki na uwezo wa kuimarisha umiliki wa mchakato wa MTAKUWWA na miundo yake ya utekelezaji ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga
• Kukuza mikakati na jitihada zenye kuimarisha ujenzi wa TAPO la wanawake na Watoto.
III. VIGEZO MUHIMU KWA WAOMBAJI WA RUZUKU
• Mashirika ya kijamii / Vikundi vya kijamii vinavyotambulika kisheria na wanaotekeleza shughuli zake ndani ya halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.
• Mashirika ya kijamii/ vikundi vya kijamii ambavyo vimekuwa wakitekeleza shughuli za MTAKUWWA katika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.
• Mashirika ya kijamii/ vikundi vya kijamii yenye mtazamo kama wa WFT - Trust katika kuondoa taratibu za kibaguzi na kuleta usawa wa kijinsia ili kuondoa udhalilishaji na ukatili kwa wanawake na Watoto, na ambao shughuli zao zinalandana na maudhui ya shirika la WFT-Trust.
• Taasisi nyingine zinazotambulika kisheria zenye uhalali na fursa za kutekeleza na / au kusimamia utekelezaji wa MTAKUWWA ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga.
IV. MADIRISHA YA UFADHILI
DIRISHA DOGO LA UFADHILI
• Kiwango cha ruzuku inayotolewa (TSH 10,000,000 – TSH 15,000,000)

• Sifa – Ruzuku katika dirisha hili zinaweza kuombwa na Mashirika / Taasisi zinazotekeleza na kusimamia mikakati ya muda mfupi ya utekelezaji wa MTAKUWWA.
DIRISHA LA KATI LA UFADHILI
• Kiwango chauzuku inayotolewa ni kati ya ( TSH 16,000,000- TSH 50,000,000)
• Muda wa kutekeleza mradi kuanzia miezi 6 hadi mwaka mmoja
• Sifa - Ruzuku katika dirisha hili zinaweza kuombwa na Mashirika / Taasisi zinazotekeleza na kusimamia mikakati ya muda wa kati katika utekelezaji wa MTAKUWWA
JINSI YA KUOMBA RUZUKU
Waombaji wa ruzuku wafuate hatua zifuatazo:
1. Kuwasilisha Andiko la Mradi (Iisilozidi kurasa 5-7) likielezea mradi pendekezwa utakaotelezwa
2. Andiko la mradi litumwe na viambatanisho vifuatavyo:
• Nakala ya cheti cha usajili cha shirika/kikundi
• Nakala ya katiba ya shirika/ kikundi
• Taarifa ya karibuni ya akaunti ya benki ya shirika/ kikundi
3. Maombi yote yatumwe kwa kutumia fomu ya muongozo wa maombi ya ruzuku inayopatikana katika tovuti ya WFT-Trust: www. wft.or.tz . Fomu pia zinapatikana katika ofisi za WFT-Trust zilizopo Jengo jipya la NSSF MAFAO House barabara ya mwanza, Ghorofa ya kwanza ( muda wa kazi)
Maombi yatumwe kwa barua barua pepe: grants@wftrust.or.tz kichwa cha habari kisomeke “NPA VAWC SHINYANGA “ Ama kwa sanduku la barua
Mkurugenzi Mtendaji, WFT-Trust, S. L. P 79235, Dar es Salaam
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464