CCM KAHAMA YAONYA RUSHWA JIMBO LA USHETU


Katibu wa CCM wilaya ya Kahama Emmanuel Mbamange


Na Salvatory Ntandu - Kahama


Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Kahama Mkoa wa Shinyanga kimesema kitawaengua watia nia wa ubunge wa jimbo la Ushetu watakaobainika kujihusisha na vitendo vya rushwa katika zoezi la uchukuaji wa fomu za kugombea ubunge wa jimbo hilo zilizoanza kutolewa leo Agosti 30,2021.


Kauli hiyo imetolewa leo na Katibu wa CCM wilaya ya Kahama Emmanuel Mbamange ambaye pia ni msimamizi wa uchaguzi mdogo wa jimbo la Ushetu wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake kuhusu zoezi la uchukuaji na urejeshaji wa fomu za kugombea ubunge ndani ya chama hicho.


Amesema watia nia watakaobainika kutoa rushwa kushawishi wajumbe ili wawapigie kura katika mchakato huo,pindi watakapothibitika chama kitawaengua katika zoezi hilo na kuwataka kujihadhari na vitendo hivyo.


“Leo Agosti 30,2021 tumeanza kutoa fomu na zinapaswa kurejeshwa septemba mosi mwaka huu saa 10 kamili jioni wanachama wote wa CCM na wanakaribishwa na fomu zinatolewa kwa gharama ya shilingi laki mmoja tu,na ofisi,”amesema Mbamange.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464