Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, katikati, akiwa na Meya wa Manispaa ya Shinyanga David Nkulila kushoto, na Katibu wa CCM wilaya ya Shinyanga Mjini Agnes Bashem kulia, wakiangalia mradi ufugaji Nguruwe wa kikundi cha Watu wenye ulemavu Kitangili Manispaa ya Shinyanga.
Na Marco Maduhu, SHINYANGA
KAMATI ya siasa ya Chama cha Mapinduzi CCM wilaya ya Shinyanga Mjini, imeridhishwa na utekelezaji wa mradi wa ufugaji Nguruwe, katika kikundi cha Mshikamano cha watu wenye ulamavu kilichopo Kitangili Manispaa ya Shinyanga.
Mwenyekiti wa Kamati hiyo Abubakari Mukadam, amebainisha hayo leo wakati akiambatana na wajumbe wake, pamoja na wataalam Manispaa ya Shinyanga, akiwamo na Mkurugenzi, kwenye ukaguzi wa mradi wa ufugaji Nguruwe, ambao unatekelezwa na watu wenye ulamavu kwa fedha za mkopo asilimia Mbili, ambazo hutolewa na Halmashauri kupitia mapato yake ya ndani.
Amesema wanawapongeza watu hao wenye ulemavu, kwa kukopa fedha hizo asilimia Mbili na kuanzisha mradi wa uzalishaji mali na kuwaingizia kipato, huku wakirejesha kwa wakati, na kuwataka waendelee kujituma kufanya kazi ili kuendesha maisha yao.
“Naipongeza sana Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga, kwa kujali makundi haya maalum na kutoa fedha za mikopo kwa watu wenye ulemavu ili kuwainua kiuchumi, na hapa mmegusa moja kwa moja ilani ya CCM kwa kusaidia makundi haya,”amesema Mukadam.
Naye, Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, akizungumza kwenye ziara hiyo, ameagiza Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga, kuacha kuwa wanakata fedha za mikopo watu hao wenye ulemavu, bali wawapatie kiwango ambacho wanakiomba na siyo kuwapa fedha Nusu.
“Fedha za mikopo ambazo wanaziomba watu hawa wenye ulemavu, wawe wanapewa zote na siyo kuwakata, kwanza wapo wachache, wapeni ili watimize malengo yao,”amesema Mboneko.
Aidha, amemtaka Mwenyekiti wa Shirikisho la chama cha watu wenye ulemavu mkoani Shinyanga(SHIVYAWATA) Richard Mpongo, kuwa kikundi chochote kile cha watu wenye ulemavu, ambacho kitapewa fedha za mkopo tofauti na kiwango walichokiomba wampatie taarifa.
Awali Mwekahazina wa kikundi hicho cha watu wenye ulemavu Janety Maganga, akisoma taarifa, amesema kikundi chao kina watu Wanne, wanajihusisha na ufugaji wa Nguruwe, ambapo awali walipewa mkopo Sh. milioni 2, na wakarejesha wote, na mwaka huu waliomba Sh, milioni 5, lakini wakapewa Sh. milioni 3 fedha ambazo wamedai kutokidhi mahitaji yao.

Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, akizungumza kwenye ziara hiyo.
Mwenyekiti wa Shirikisho la chama cha watu wenye ulemavu (SHIVYAWATA) Mkoani Shinyanga, Richard Mpongo, akizungumza kwenye ziara hiyo ya kamati ya siasa ya CCM.
Mwekahazina wa kikundi cha watu wenye ulamavu Janety Maganga, akisomaa taarifa ya kikundi hicho cha ufugaji wa Nguruwe kwa kutumia kitabu cha Nukta Nundu.
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, katikati, akiwa na Meya wa Manispaa ya Shinyanga David Nkulila kushoto, na Katibu wa CCM wilaya ya Shinyanga Mjini Agnes Bashem kulia, wakiangalia mradi ufugaji Nguruwe wa kikundi cha Watu wenye ulemavu Kitangili Manispaa ya Shinyanga.
wajumbe wa Kamati ya Siasa ya chama cha mapinduzi CCM wilaya ya Shinyanga mjini, wakipiga picha ya pamoja na kikundi cha Ujasiriamali cha watu wenye ulemavu.
Na Marco Maduhu- Shinyanga.
Na Marco Maduhu- Shinyanga.