Wanachadema Jimbo la Shinyanga Mjini wakiwa katika maombi ya kumuombea Mwenyekiti wao wa Taifa Freeman Mbowe na wenzake ambao wapo Mahabusu.
Na Marco Maduhu, SHINYANGA.
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Jimbo la Shinyanga Mjini, kimeendesha maombi maalum ya kumuombea Mwenyekiti wa chama hicho Taifa Freeman Mbowe pamoja na wenzake, ambao wapo mahabusu wakikabiliwa na tuhuma mbalimbali zikiwamo ugaidi na uhujumu uchumi.
Maombi hayo yamefanyika leo kwenye Ofisi cha Chadema Kanda ya Serengeti Mjini Shinyanga, yakiongozwa na Mchungaji Mussa Kagoma kutoka Kanisa la Matengenezo.
Mwenyekiti wa Chadema Jimbo la Shinyanga Mjini Hamis Ngunila, akizungumza mara baada ya kumalizika kwa maombi hayo, amewataka wanachadema waendelee kusimama imara, licha ya kukabiliwa changamoto mbalimbali za kisiasa, ikiwamo kukamatwa viongozi wao wa ngazi za juu.
“Ndugu zangu misukosuko ambayo wanapitia viongozi wetu, ni njia ya kutuzoofisha, na kututoa kwenye njia ya kudai Katiba Mpya, hivyo tusikate tamaa tuendelee kusimama imara na kukipigania chama,”amesema Ngunila.
“Chadema jimbo la Shinyanga mjini tumejipanga kufanya makongamano ya kudai Katiba Mpya kwenye Kata zote 17 za mjini Shinyanga, na Katiba ndiyo itakuwa salama kwetu sisi na watanzania wote hasa kwenye suala la upataji haki,”ameongeza Ngunila.
Naye, Katibu wa Baraza la wanawake mkoa wa Shinyanga (BAWACHA) Agata Mamuya, amewataka wanachadema kusimama imara pamoja na Mwenyekiti wao Taifa Freeman Mbowe, na kumuombea dhidi ya kesi ambazo zinamkabili ashinde na kuachiwa huru
Kwa upande wake Mchungaji wa Kanisa la Matengenezo la Mjini Shinyanga Mtume Mussa Kagoma, akizungumza kabla ya kuendesha maombi, amewataka viongozi wawe waumini wa kutenda haki, ili kuendelea kudumisha amani ya nchi.

Mchungaji wa Kanisa la Matengenezo Shinyanga Mjini Mtume Mussa Kagoma, akiongoza maombi ya kumuombea Mwenyekiti wa Chadema Taifa Freeman Mbowe.
Maombi yakiendelea.
Maombi yakiendelea.
Mwenyekiti wa Chadema Jimbo la Shinyanga Mjini Hamis Ngunila, akizungumza na Wanachadema, mara baada ya maombi kumalizika.
Mwenyekiti wa Chadema Jimbo la Shinyanga Mjini Hamis Ngunila, akiendelea kuzungumza na Wanachadema wa Jimbo hilo.
Katibu wa Baraza la Wanawake Chadema BAWACHA Mkoa wa Shinyanga Agatha Mamuya, akizungumza na Wanachadema, mara baada ya kumalizika kwa maombezi maalum ya kumuombea Mbowe.
Wanachadema wakiwa kwenye maombezi maalum ya kumuombea Mbowe, pamoja na kusikiza Nasaha za viongozi wao.

Na Marco Maduhu- Shinyanga.
Na Marco Maduhu- Shinyanga.