DC MBONEKO AKAGUA MATENGENEZO TAA ZA BARABARANI...SHINYANGA MJINI USIKU KAMA MCHANA


Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, akizungumza mara baada ya kumaliza kukagua matengezo ya Taa za Barabarani Mjini Shinyanga.

Na Marco Maduhu, Shinyanga

Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko, amekagua matengenezo ya taa za barabarani za Manispaa ya Shinyanga.


Taa za barabarani mjini Shinyanga zilizimika tangu mwaka jana 2020 kuanzia Septemba na Oktoba kutokana na kupata hitilafu, ambapo Serikali ili kaa na Mkandarasi Jasco na kumuagiza azifanyie marekebisho ya haraka.

Akizungumza wakati wa ukaguzi wa matengenezo ya taa hizo, Mboneko amesema kwa sasa mji wa Shinyanga ung'aa na hakuna tena giza, pamoja na wananchi kufanya biashara muda wote sababu ya mwanga.

"Nimekagua matengenezo ya Taa hizi za Barabarani, ambapo Serikali tumetoa siku 10 tu, taa zote ziwe zinawaka, na tumeona kasi ya Mkandarasi na tuna imani atakamilisha ndani ya wakati,"amesema Mboneko.

Aidha, Mboneko amesema wataendelea kuzikagua taa hizo kila siku, na zile ambazo zitakuwa zikizimika, watakuwa wakizifanyia marekebisho ili kuhakikisha hakutakuwa na giza tena.

Naye,msimamizi wa Kampuni ya Jasco Ismail Mussa, ambaye anasimamia matengezo ya taa hizo, amesema awali taa zilizimika kutokana na kuwa na hitilafu kwenye Betri, lakini kwa sasa taa walizozileta ni imara zaidi.

Kwa upande wake Meneja Wakala wa Barabara Mjini na Vijijini TARURA Manispaa ya Shinyanga Salvatory Yambi, amesema mpaka sasa zimeshafungwa taa 241, kati ya taa 438, ambapo zoezi hilo bado linaendelea la ufungaji wa taa hizo.

Nao baadhi ya wafanyabiashara wameipongeza Serikali, kwa kufanya matengenezo ya taa hizo, ambazo zimewasaidia kufanya biashara zao usiku katika maeneo yenye mwanga, pamoja na kuwapunguzia gharama za kununua betri ama kukodi tochi kwa ajili ya kumulika bidhaa zao.
 

Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko, akizungumza mara baada ya kumaliza kukagua matengezo ya taa za Barabarani Mjini Shinyanga.

Meneja Wakala wa Barabara Mjini na Vijijini TARURA Manispaa ya Shinyanga Mhandisi Salvatory Yambi, akielezea hatua ilipofikia Matengenezo ya taa za Barabarani.

Diwani wa Masekelo Peter Kwoliba, akielezea namna wananchi walivyofurahi mara baada ya taa hizo kuanza kuwaka tena.

Msaidizi wa Kampun ya Jasco Ismail Mussa, akielezea hatua ambayo wamefikia kwenye ufungaji wa Taa hizo.

Mfanyabashara Emmaculate Raphael katika eneo la barabara ya Ngokolo Mitumbani, akielezea namna anavyofanyika biashara zake usiku bila ya wasiwasi wowote kutokana na kuwapo na taa za Barabarani.

 

Wafanyabiashara wakiendelea na biashara zao,usiku sababu ya kuwapo na Taa za Barabarani, ambapo suku kama mchana.

Biashara zikiendelea usiku katika maeneo mbalimbali ya Shinyanga Mjini, wa pili kutoka Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko, akishuhudia biashara zikiendelea jirani na Taa za Barabarani ambapo kuna Mwanga.


Biashara zikiendelea usiku kama mchana.

Biashara zikiendelea usiku kama mchana.

 

Awali Mafundi wakiendelea na Matengenezo ya ufungaji wa Taa za Barabarani kuanzia Mchana hadi Usiku.

 

Zoezi la matenegezo ya ufungaji Taa za Barabarani Mjini Shinyanga likiendelea huku likishuhudiwa na Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, wapili kutoka kulia.


Na Marco Maduhu- Shinyanga

Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464