Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, akizungumza kwenye ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa Daraja la Iwelyangula ambalo linaunganisha Kata za Chamaguha na Kitangili.
Na Marco Maduhu, SHINYANGA.
MKUU wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, amekemea tabia ya baadhi ya wananchi kufanya shughuli za kilimo Kandokando ya barabara, hali ambayo ina sababisha uharibifu wa miundombinu hiyo yakiwamo Madaraja.
Mboneko ametoa onyo hilo leo, wakati akikagua maendeleo ya ujenzi wa daraja la Iwelyangula, ambalo lina unganisha Kata mbili za Chamaguha na Kitangili zilizopo Manispaa ya Shinyanga.
Alisema ni marufuku wananchi kufanya shughuli za kilimo kando kando ya miundombinu ya barabara, bali walime kwenye maeneo ya mashamba, ili kuzuia uharibifu wa miundombinu hiyo, ambayo imekuwa ikiigharimu Serikali kwa kutumia fedha nyingi za matengenezo, ambazo zinge elekezwa kwenye miradi mingine ya maendeleo.
“Nimarufuku wananchi kulima Kando ya barabara, kalimeni huko kwenye Mashamba, mnatuhalibia barabara zetu na kuingiza gharama Serikali, na aagiza pia viongozi wa maeneo haya, wananchi ambao wamelima Kando ya Barabara hii, wavume mazao yao na wasilime tena, ili kuilinda barabara na daraja hili,”alisema Mboneko.
“Mwezi wa Sita mwaka huu, nilifika kwenye hili daraja na kukuta limebomoka, na wananchi wa Kata hizi mbili za Chamaguha na Kitangili kukosa mawasiliano, ndipo nikapiga Simu kwa Mtendaji Mkuu wa TARURA na kupewa Sh, milioni 428 kwa ajili ya kujenga daraja jipya ambalo ni bora zaidi,”aliongeza Mboneko.
Aidha, Mboneko alisema mbali na ujenzi wa daraja hilo, pia TARURA wameamua kujenga na miundombinu ya barabara Kilomita 1.6 kwa kiwango cha Changalawe, ambayo inaunganisha Kata hizo mbili za Chamaguha na Kitangili kupita kwenye daraja hilo jipya.
Kwa upande wake Meneja wakala wa barabara Mjini na Vijijini (TARURA) Manispaa ya Shinyanga Mhandisi Salvatory Yambi, alisema ujenzi wa daraja hilo ulianza June utakamilika Septemba 30 mwaka huu.
Nao baadhi ya wananchi wa Kata hizo mbili akiwamo Bahati Samali, waliipongeza Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, kwa kuwasaidia ujenzi wa daraja hilo, ambalo ni kiungo chao muhimu katika shughuli za kiuchumi, na kupata huduma za afya.
Pia, wanafunzi ambao wanaishi Chamaguha na kusoma Kitangili, ambao huvuka daraja hilo akiwamo Agnes Dotto, walisema kipindi cha masika hulazimika kubaki nyumbani sababu ya kuhofia kusombwa na maji, lakini daraja hilo litakapo kamilika hawatakosa tena vipindi vya Masomo.

Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, akizungumza wakati akikagua maendeleo ya ujenzi wa daraja Jipya ambalo linaunganisha Kata ya Chamaguha na Kitangili.
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, akizungumza na baadhi ya wananchi wakati akikagua maendeleo ya ujenzi wa daraja hilo na kuwaonya kulima kando kando ya Barabara.
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, akizungumzia ujenzi wa daraja hilo.
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, akiwa na baadhi ya viongozi kwenye daraja hilo.
Ukaguzi maendeleo ujenzi wa daraja ukiendelea.

Muonekao wa daraja la Iwelyangula, ambalo linaunganisha Kata za Chamaguha na Kitangili.
Mafundi wakiendelea na ujenzi wa Daraja.
Ukaguzi wa daraja na Miundombinu ya barabara ukiendelea.
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, kushoto akiwa na Diwani wa Chamaguha Elias Masumbuko, wakibadilishana mawili matatu, wakati wa ukaguzi wa maendeleo ya ujenzi wa daraja hilo.
Diwani wa Chamaguha Elias Masumbuko, akielezea umuhimu wa daraja hilo, hasa katika masuala ya kukuza uchumi.
Diwani wa Kitangili Manispaa ya Shinyanga Mariam Nyangaka, akizungumzia umuhimu wa daraja hilo, ambalo linaunganisha Kata za Chamaguha na Kitangili.
Mwananchi Bahati Samali, akitoa pongeza kwa Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, kuwasaidia ujenzi wa daraja hilo.
Awali Meneja Wakala wa Barabara Mjini na vijijini TARURA Manispaa ya Shinyanga Mhandisi Salvatory Yambi, akisoma taarifa ya ujenzi wa daraja hilo.
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, awali akiwa katika Ziara ya kukagua miundombinu ya barabara na ujenzi wa daraja jipya ya Iwelyangula, ambalo linaunganisha Kata za Chamaguha na Kitangili Manispaa ya Shinyanga.
Na Marco Maduhu, SHINYANGA.
Na Marco Maduhu, SHINYANGA.